Home Habari za michezo GIBBS – WHITE AONYESHA JERAHA LAKE AKIMTAJA MWENZAKE

GIBBS – WHITE AONYESHA JERAHA LAKE AKIMTAJA MWENZAKE

0

LONDON, ENGLAND: MORGAN Gibbs-White ametumia mitandao ya kijamii kuwashukuru mashabiki baada ya kupokea ujumbe mwingi wa pole kufuatia jeraha baya la kichwa alilolipata katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea, uliomalizika kwa kichapo cha mabao 3-1.

Kiungo huyo wa Nottingham Forest alichapisha picha akiwa na nyuzi alizoshonwa kwenye paji la uso wake, zikionyesha ukubwa wa jeraha hilo linalomuweka shakani kucheza katika nusu fainali ya pili ya Europa League dhidi ya Aston Villa, kesho Alhamisi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Gibbs-White aliandika: “Asanteni kwa ujumbe wa faraja, ushindi mkubwa, hongera Taiwo Awoniyi.”

Forest waliendelea kuwa kwenye kiwango bora licha ya kichapo hicho, wakiwa na mfululizo wa mechi 10 bila kupoteza katika mashindano yote. Katika mchezo huo, mshambuliaji Taiwo Awoniyi alifunga mabao mawili huku Igor Jesus akiongeza moja kwa penalti.

Hata hivyo, timu hiyo ilipata pigo kubwa baada ya kumpoteza Gibbs-White, ambaye alipata jeraha hilo katika kipindi cha pili, dakika 20 tu baada ya kuingia akitokea benchi.

Kocha wa Forest, Vitor Pereira amesema bado anasubiri taarifa kamili ya madaktari kuhusu hali ya mchezaji huyo.

“Gibbs-White ana jeraha kubwa, lakini ni mpiganaji. Natumaini madaktari watafanya kila wawezalo ili awe tayari kucheza dhidi ya Villa. Anazungumza vizuri na anakumbuka kila kitu, tatizo ni maumivu tu,” amesema Pereira.

Forest pia walimpoteza beki Zach Abbott kutokana na jeraha la kichwa, lakini kocha huyo amesema anaendelea vizuri.

Pereira alifanya mabadiliko manane katika kikosi chake dhidi ya Chelsea, akijiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Aston Villa ambapo Forest wanaongoza kwa bao 1-0.