Mchezo ulikuwa wa kasi na wa kuvutia na hakukuwa na upande uliokuwa na wasiwasi wa kujibaoa nyuma na mastaa wote walikuwa na nia ya kushambulia. Ilionekana kama mpira ulikuwa hauishi uwanjani, mchezo ukifanana na mpira wa kikapu wenye mashambulizi ya mfululizo.
MPIRA UWANJANI
Kwa muda wa mpira kuwa uwanjani ilikuwa asilimia 54.9 ya mchezo, chini kidogo ya wastani wa Ligi ya Mabingwa msimu huu (58.3%).
Lakini hilo linaweza kuelezwa zaidi na idadi kubwa ya mabao. Zaidi ya dakika 10 zilipotea kutokana na sherehe za mabao na ucheleweshaji wa kuanza upya mchezo.
Tukitazama maeneo ya mchezo ambayo wachezaji wanaweza kudhibiti moja kwa moja, mojawapo ilionekana wazi kwamba mipira ya kurusha (throw-ins).
PSG na Bayern walichukua sekunde 13.7 kuanza tena mchezo baada ya kurusha, haraka kuliko timu yoyote ya Ligi Kuu England msimu huu (Manchester City ndio wana haraka zaidi kwa sekunde 14.9).
Katika dunia (hasa Ligi Kuu England) ambako ulimwengu unazidi kuona timu zikichelewa kurusha mipira mirefu ndani ya eneo la hatari, ilikuwa faraja kuona timu mbili zikiwa na haraka ya kurudisha mpira uwanjani.
Mapema mwezi huu, rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis, alipendekeza mabadiliko makubwa yenye lengo la kuboresha soka ili kuvutia kizazi kipya na bilionea huyo mwenye umri wa miaka 76 alisema mfumo wa sasa wa dakika 90 ni mrefu sana kwa kizazi kilichokulia kwenye michezo ya video, akipendekeza kupunguzwa kwa muda wa vipindi na kuondolewa kwa kadi za njano na nyekundu.