DAR City inatarajiwa kucheza na Petro de Luanda ya Angola katika mechi ya robo fainali ya Basketball African League (BAL) ikitajwa itakuwa vita ya kisasi.
Robo fainali ya BAL inatarajiwa kuanza Mei 22-31 nchini Rwanda ikizikutanisha timu nne zilizofuzu katika kundi la Kalahari Conference na nne kutoka Sahara Conference.
Mechi hiyo ya play-off Dar City itaingia na kumbukumbu ya kufungwa na Petro kwa pointi 100-75 katika Ligi ya Afrika iliyofanyika Afrika Kusini.
Moja ya rekodi nzuri za Dar City nikutokuruhusu kufungwa mara mbili na timu moja kama ilivyokuwa dhidi ya Johannesburg Giants ya Afrika Kusini.
Katika mechi ya kwanza mashindano ya Road to BAL Elite 16 ya Kenya, ilifungwa pointi 71-69, kabla ya kulipa kisasi na kushinda 100-70 katika Ligi ya Afrika BAL, Afrika Kusini.
Katika Ligi ya Afrika, Petro ilimaliza ya kwanza huku Dar City ikimaliza ya nne na hivyo mabingwa hao wa BDL, watakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha inashinda na kutinga nusu fainali.
Robo fainali nyingine itazikutanisha Al Ahly ya Misri dhidi ya Ville de Dakar ya Senegal, Club African (Tunisia) vs Al Ahly (Libya), RSSB Tigers (Rwanda) vs Fus Rabat (Morocco)
Katika mashindano haya, Petro ndiyo timu iliyocheza mara nyingi hatua hii tangu yalipoanza mwaka 2021, ikimaliza ya nafasi ya tatu baada ya kufungwa na Zamalek ya Misri iliyotinga fainali.
Pia ilimaliza nafasi ya pilimwaka 2022 baada ya kufungwa na Monastir ya Tunisia katika fainali na mwaka 2024 ikamaliza ya nne na mwaka 2025 ya pili.
Kwa upande wa Dar City, hii ndiyo mara ya kwanza kucheza robo fainali na kwa sasa ikiwa chini ya Kocha Mamadou Gueye kutoka Senegal, Mohamed Mbwana na Nabil Kabalan, inajifua kwenye Uwanja wa Donbosco, Oyster bay.
ROBO FAINAL-BAL PLAY OFF
Dar City (Tanzania) vs Petro de Luanda (Angola).
Al Ahly Ly (Libya) vs Club Africain (Tunisia)
Al Ahly (Misri) vs Ville de Dakar (Senegal)






