Habari za michezo
AS ROMA NA PRESHA YA KUFUZU LIGI YA MABINGWA ULAYA
Vardo
May 10, 2026
3:09 pm
Leo Mei 10 saa 7:00 usiku, Uwanja wa Ennio Tardini utakuwa mwenyeji wa mchezo wa Serie A kati ya Parma inayo shika nafasi ya 12 na AS Roma nafasi iliyopo ya 5.
Roma wakiwa na pointi 64 wanashindana kwa nafasi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakiwa wana pointi moja tu nyuma ya Milan wa nafasi ya 3 na nyuma ya Juventus kwa pointi mbili.
Kwa upande mwingine, Parma wakiwa na pointi 42 wamejihakikishia usalama wa kukaa Serie A na wanatafuta kumaliza katika nafasi za juu zaidi katika michezo mitatu iliyosalia.
AS Roma wanarekodi ya michezo mitano bila kufungwa, ikiwemo ushindi mkubwa wa 4-0 dhidi ya Fiorentina wiki iliyopita . Hata hivyo, wana wasiwasi mkubwa wa majeruhi nahodha Lorenzo Pellegrini ana uwezekano mdogo wa kucheza kwani bado anapona jeraha la mguu, pamoja na Artem Dovbyk na Lewis Ferguson ambao wamo nje.
Upande wa Parma, wana majeruhi wa muda mrefu kama Frigan na Cremaschi, lakini hawana wachezaji waliopigwa marufuku au kusimamishwa kutokana na adhabu.
Kihistoria, AS Roma wana ubabe mkubwa dhidi ya Parma, wakiwa wameshinda mara 26 kwenye michezo 34 ya hivi karibuni huku Parma wakiwa na ushindi 4 pekee na sare 4 . Katika michezo mitano ya mwisho ya Ligi Kuu kati ya timu hizi, Roma wameshinda mara nne na Parma mara moja. Ushindi wa mwisho wa Parma nyumbani kwao dhidi ya Roma ulikuwa mwaka 2021, wakati walishinda 2-0 . Mchezo wa mwisho kati yao Oktoba 2025 ulimalizika 2-1 kwa Roma.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Parma wanatarajiwa kupanga mfumo wa 3-5-1-1 chini ya kocha Carlos Cuesta, na Zion Suzuki akiwa langoni, huku Adrian Bernabé akiwa mhimili wa kiungo na Mateo Pellegrino akiwa mshambuliaji mkuu . Roma wakitumia mfumo wa 3-4-2-1 wa Gian Piero Gasperini, wakiwa na Mile Svilar langoni, na Donyell Malen anatarajiwa kuwa mshambuliaji mkali wakiwa nyumbani . Wachezaji kama Paulo Dybala na Leandro Paredes wanatarajiwa kuanza kwenye benchi na kuingia baadaye.
Kwa kuzingatia ubora wa Roma na hitaji lao la pointi za kufuzu Champions League, wana nafasi kubwa ya ushindi. Hata hivyo, Parma wakiwa nyumbani wana rekodi ya kupambana kwa ushupavu, wakiwa wamepoteza michezo 7 tu kati ya 17 nyumbani msimu huu. Jisajili