Habari za michezo

WANAMICHEZO WALIVYONG’ARA TUZO ZA BMT

Vardo May 10, 2026 5:39 pm

TUZO za Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ambazo hutolewa ili kutambua mchango wa wanamichezo bora nchini, zimefanyika usiku wa Mei 9, 2026 katika ukumbi wa The Super Dome Masaki uliopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni msimu wa nne mfululizo tangu zilipoanza 2022.Katika hafla hiyo, tuzo zilitolewa kwa makundi mbalimbali ambayo ni mwanamichezo bora wa kiume na kike, mwanamichezo bora kijana wa kiume na kike, mwanamichezo bora wa kiume na kike mwenye ulemavu, timu bora ya taifa wanaume na wanawake, timu bora ya klabu wanawake na wanaume, kocha bora wa kiume na wa kike, mwanamichezo bora wa kike na kiume kutoka shuleni, mwamuzi bora wa kiume na wa kike, mwanahabari za michezo bora wa kiume na wa kike, mwanamichezo nguli wa zamani ‘Sports Legend Award’, mwanahabari nguli wa michezo pamoja na tuzo ya mchezaji bora chaguo la watu mwanaume na mwanamke.

Katika utoaji wa tuzo hizo za mwaka 2025 ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mwigulu Lameck Nchemba, kulikuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wanamuziki na ngoma za asili.Mbali na wanamichezo na timu kupewa tuzo, pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan alipongezwa kwa uongozi wake mahiri, dira pana na dhamira ya dhati ya kuwekeza katika sekta ya michezo ambapo chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, sekta hiyo imepiga hatua kubwa ambazo leo zinashuhudiwa kwa fahari, kuongezeka hamasa, ushindani na mafanikio ya timu na wanamichezo mbalimbali katika anga za kitaifa na kimataifa. Kutokana na hilo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda alimkabidhi Mwigulu Nchemba, Tuzo ya Heshima ya Rais Samia kama ishara ya kutambua mchango wake mkubwa katika kuendeleza na kuinua sekta ya michezo nchini Tanzania.

AS ROMA NA PRESHA YA KUFUZU LIGI YA MABINGWA ULAYA MASTAA AZAM WAUGUA GHAFLA