Habari za michezo

HALI YA KIKOSI YANGA YAFICHULIWA KABLA YA MECHI

Vardo May 13, 2026 9:01 am

WAKATI presha ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma Jiji FC ikiendelea kupanda, kambi ya Yanga SC imepokea taarifa njema baada ya daktari wa timu hiyo, Moses Etutu, kuthibitisha kuwa kikosi kiko katika hali nzuri na wachezaji wengi wako tayari kwa pambano hilo muhimu la kusaka alama tatu.

Etutu amesema kwa sasa hakuna majeraha mapya ndani ya kikosi hicho, huku akibainisha kuwa ni Dickson Job na Clement Mzize pekee wanaoendelea na programu maalum za matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji hivi karibuni.

Kwa mujibu wa daktari huyo, maendeleo ya wawili hao yanaendelea vizuri chini ya uangalizi wa idara ya tiba pamoja na benchi la ufundi, jambo linalotoa matumaini ya kuwaona wakirejea uwanjani wakiwa katika ubora wao baada ya kukamilisha programu za kujiweka sawa.

Ameongeza kuwa hali ya wachezaji wengine ni nzuri, morali ipo juu kambini na kila mmoja anaelekeza nguvu zake katika kuhakikisha timu inaendelea kupata matokeo chanya katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi msimu huu.

“Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya kusaka alama tatu muhimu dhidi ya Dodoma Jiji FC. Tunajua ushindani uliopo, lakini kikosi kiko tayari kupambana,” amesema Etutu.

Yanga inatarajiwa kushuka dimbani leo kwenye Uwanja wa Airtel ikiwa na dhamira ya kuendeleza rekodi yao ya kutofungwa msimu huu katika Ligi Kuu Tanzania Bara. Mashabiki wa timu hiyo pia wanatarajia kuona muendelezo wa kiwango bora na kasi ambayo timu imekuwa ikiionyesha tangu kuanza kwa msimu huu

KAGOMA AFURAHI KURUDI KIGOMA, AITAMANI DAKIKA 90 DHIDI YA MASHUJAA MASHUJAA WAMEINGIA KWENYE HESABU ZA SIMBA, MATOLA ATOA ONYO