Habari za michezo
HIZI NDIZO JOZI ZINAZOFANYA SIMBA KUWA HATARI
Vardo
May 13, 2026
6:04 pm
MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, ameweka wazi kuwa siri ya uimara wa timu hiyo haipo kwa mchezaji mmoja pekee, bali ni ubora wa kombinesheni mbalimbali ndani ya kikosi chao.
Ahmed amesema miongoni mwa jozi zinazovutia zaidi ndani ya Simba kwa sasa ni ushirikiano kati ya Elie Mpanzu na Clatous Chama, ambao wamekuwa wakionesha kiwango kikubwa kila wanapopata nafasi ya kucheza pamoja.
Kwa mujibu wake, wawili hao wanaelewana vizuri uwanjani na mara nyingi huifanya Simba kuwa hatari zaidi kwenye eneo la ushambuliaji.
Mbali na Mpanzu na Chama, Ahmed Ally pia amezitaja kombinesheni nyingine ambazo zimekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho, akiwemo ushirikiano wa Anicet Oura na Kibabage pamoja na ule wa Yusuph Kagoma na Alasane Kante.
Amesema kila mchezaji ndani ya kikosi ana nafasi yake muhimu katika mafanikio ya timu.
Meneja huyo ameeleza kuwa Simba imekuwa ikipewa nguvu zaidi na maelewano mazuri ya baadhi ya wachezaji wanaocheza kwa ukaribu, akiwataja Libasse Gueye na Shomari Kapombe kuwa miongoni mwa wachezaji wanaosaidiana vizuri wanapokuwa ndani ya uwanja.
Ahmed pia amewataja Rushein De Reuck na Ismael Toure kuwa sehemu ya mchanganyiko muhimu unaoifanya Simba kuwa timu yenye ushindani mkubwa msimu huu.
Amesema uimara wa kikosi hicho unatokana na uwezo wa wachezaji kuelewana haraka na kusaidiana katika nyakati tofauti za mchezo.
“Hii ni kombinesheni hatari sana, wakiwepo hapo ndani ya kikosi kimoja Simba inakuwa tishio,” amesema Ahmed
Huku akisisitiza kuwa mafanikio ya Simba yanatokana na ushirikiano wa kila idara ndani ya timu, kuanzia safu ya ulinzi, kiungo hadi ushambuliaji.