Habari za michezo

OKELLO MCHEZAJI BORA WA MWEZI APRILI

Vardo May 13, 2026 6:10 pm

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Allan Okello amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Aprili wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuonesha kiwango bora katika michezo ya mwezi huo.

Okello ameibuka na tuzo hiyo baada ya kuwa na mchango mkubwa kwa timu yake katika michezo mitatu aliyocheza, ambapo amefunga bao moja na kutoa pasi sita za mabao.

Kiungo huyo raia wa Uganda ameendelea kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa Yanga katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi msimu huu kutokana na ubunifu wake uwanjani pamoja na uwezo wa kutengeneza nafasi za mabao.

Hivi karibuni alichaguliwa pia, na klabu yake kuwa mchezaji bora wa NIC Insurance ikiwa ni utaratibu waliyojiwekea klabu hiyo ya kutoa tuzo kwa wachezaji wao wanaofanya vizuri kila mwezi.

Tangu ajiunge na Yanga Januari mwaka huu kwa ujumla amecheza michezo 15ya Ligi Kuu akihusika katika mabao 12 na kutoa pasi za mabao saba.

HIZI NDIZO JOZI ZINAZOFANYA SIMBA KUWA HATARI