Habari za michezo
TOURE AWEKA WAZI, SIMBA SC HAKUNA MZAHA NA MBIO ZA UBINGWA
Vardo
May 15, 2026
4:38 pm
Beki wa Simba SC, Ismael Olivier Toure, amesema mchezo wa jana dhidi ya Mashujaa FC ulikuwa na uzito mkubwa sana kwake binafsi pamoja na kikosi kizima kutokana na ushindani mkali unaoendelea kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi.
Toure ameeleza kuwa uwepo wa Yanga SC kileleni mwa msimamo wa ligi ulifanya mchezo huo kuwa na presha kubwa, huku kila timu ikihitaji matokeo chanya ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuendelea kusalia kwenye mbio hizo.
Beki huyo amesema kila mchezaji wa Simba SC alilazimika kujitoa kwa nguvu zote uwanjani, akisisitiza kuwa hakuna aliyeingia uwanjani kwa mzaha kutokana na umuhimu wa pointi zilizokuwa zinagombaniwa.
Toure amesema sasa macho yote ya kikosi hicho yameelekezwa kwenye mchezo ujao wa Jumapili, ambao nao ameutaja kuwa ni muhimu kama ule wa hivi karibuni, kwani unaweza kuamua mwenendo wa safari yao ya msimu huu.
“Simba SC ni timu kubwa yenye historia na matarajio makubwa, kila mchezaji anatakiwa kudumisha umakini, nidhamu na kujituma ili kuhakikisha mashabiki wanaendelea kupata furaha,” amesema.
Toure amesisitiza kuwa hawana muda wa kupoteza wala kuruhusu makosa ya kizembe, bali wanapaswa kupambana kwa kila dakika ili kuendelea kubaki kwenye ushindani wa juu wa ligi na kufikia malengo yao ya msimu.