Habari za michezo

DAKIKA 50 ZAMTOSHA NEYMAR KUVUTA MABILIONI

Vardo May 21, 2026 9:16 am

SAO PAOLO, BRAZIL: STAA wa kimataifa wa Brazil na Santos, Neymar Jr, amesherehekea kuitwa kwake kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia kwa kuingiza kiasi kikubwa cha fedha kupitia mitandao ya kijamii.

Ndani ya dakika 50 tu baada ya tangazo la kocha Carlo Ancelotti, Neymar alichapisha matangazo matatu ya kibiashara kwenye mitandao ya kijamii akitangaza biashara za maji, kampuni ya mavazi ya michezo na kinywaji cha kuongeza nguvu.

Kwa mujibu wa Globo, machapisho hayo matatu ya udhamini yalimuingizia Neymar kiasi cha Pauni 4.5 milioni (takriban Sh11 bilioni). Akizungumza kuhusu kikosi chake cha Kombe la Dunia, kocha Ancelotti alisema hana wasiwasi juu ya wachezaji aliowatangaza siku mbili zilizopita na kwamba kila kitu kipo juu kuamua hatima ya taifa lao.

“Sina hofu kusema kwamba tunataka kushinda Kombe la Dunia kwa sababu matarajio ni makubwa,” alisema kocha huyo raia wa Italia na kuon geza: “Tutakuwa na kikosi chenye uwezo wa kucheza soka bora, chenye moyo wa ushindani pamoja na ubora wa kipekee. Siyo kikosi kamili, nina uhakika na hilo, lakini ni bora na ni bora zaidi.

“Lazima niseme kwamba timu inayoshinda Kombe la Dunia haitakuwa timu kamili, timu kamili haipo. Timu yenye uwezo mkubwa wa kuvumilia changamoto ndiyo inaweza kushinda. Tunataka kuwa timu yenye uimara mkubwa zaidi duniani.”

MVUTANO WA MBAPPE, VINI BALAA REAL MADRID