Habari za Yanga
Yanga SC

SKAUTI WA FIFA AGOMA KUSEPA TZ KISA ‘MAVITU’ YA OKELLO…KAULI YAKE HII HAPA…

admin May 25, 2026 6:33 pm

SKAUTI mwenye leseni ya FIFA, Cedric Vanrenterghem ameamua kubadilisha ratiba yake ya kurejea Ubelgiji baada ya kuvutiwa kwa kiwango cha kiungo mshambuliaji wa Yanga na timu ya taifa ya Uganda, Allan Okello.

Badala ya kurejea Ubelgiji jana, Jumapili kama alivyopanga awali, sasa ameongeza muda wake ili kumtazama kwa karibu zaidi katika mechi mbili za kimataifa akiwa na Uganda.

Cedric ambaye anafanya kazi na kampuni ya Cherry Sports, ameonyesha kuvutiwa na Okello baada ya mchezaji huyo kuonesha kiwango cha juu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Black Stars ambapo aliweka rekodi ya aina yake.

Okello mwenye mabao tisa na asisti saba, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza katika Ligi Kuu Bara kufunga mabao mawili katika mechi tatu mfululizo. Alifanya hivyo dhidi ya Coastal Union, akaendeleza dhidi ya Tanzania Prisons na kisha akathibitisha ubora wake tena dhidi ya Singida Black Stars.

“Natamani kumuona zaidi kabla ya kuchukua hatua nyingine. Nilikuwa hapa kwa ajili ya mapumziko tu lakini yule kijana mwenye jezi namba 20 amenivutia sana. Tunaweza kuona cha kufanya baada ya kumfuatilia kwa karibu zaidi na kufahamu nani ana msimamia,” amesema.

Okello, mwenye umri wa miaka 25, alijiunga na Yanga katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari akitokea klabu ya Vipers ya Uganda, ambako alifunga mabao matatu.

Yanga inatarajiwa kushuka dimbani tena leo Jumatatu katika mbio za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara huku Okello akiwa sehemu muhimu ya kikosi. Baada ya hapo, ataungana na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Uganda kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki za kimataifa.

Timu ya taifa ya Uganda, chini ya kocha Paul Put, itacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Tanzania Juni 5, kisha siku tatu baadaye watarudi uwanjani kucheza dhidi ya Madagascar wakiwa nyumbani.

Kwa mujibu wa taarifa, inaelezwa kuwa Cedric anatarajiwa pia kufanya kikao na kocha Put ambaye ni raia wa Ubelgiji, kujadili kwa kina maendeleo ya kiungo huyo mshambuliaji.

EDO KUMWEMBE:- MPAKA SASA CHAMA 2, SIMBA 1….YANGA WANAJIFICHA KWA AIBU…. MHHH HAYA YA MSUVA HUKO IRAQ 🫣🫣🫣….AU NDIO MWISHO WA ENZI..?