Simba SC

POINTI ZA SIMBA ZAMLIZA BEKI DODOMA

Vardo May 27, 2026 11:19 pm

BEKI wa Dodoma Jiji, Andy Bikoko, ameonekana kuhuzunishwa vikali jinsi kikosi hicho kilivyopoteza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba kwa kufungwa bao 1-0.

Mechi hiyo iliyochezwa Mei 24, 2026 kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, bao la Simba lilifungwa dakika ya 62 na Elie Mpanzu aliyemalizia mpira uliopanguliwa na kipa Daniel Mgore, kufuatia Clatous Chama kupiga penalti.

Akizungumza na Mwanaspoti, Bikoko alisema kama Simba ikiwa bingwa msimu huu, basi itakuwa imenufaika na pointi tatu ambazo hazikuwa halali walizopata kwenye mchezo dhidi yao.

Bikoko alisema msimu huu wamekuja tofauti dhidi ya timu kubwa kutokana na Dodoma Jiji kuwa na wachezaji bora na kocha ambaye aliwapa mbinu sahihi za kutokuwa na hofu dhidi ya vigogo.

“Simba walipata ushindi kutokana na penalti nyepesi ambayo haikuwa halali, lakini pili kulikuwa na makosa wakati wa upigwaji wa penalti hiyo kwa Mpanzu na wachezaji wengine kuingia ndani ya eneo la hatari kabla ya kupigwa,” alisema Bikoko.

Kwa anachokililia Bikoko, video za tukio hilo zinaonyesha wakati Chama anajiandaa kupiga penalti huku wachezaji wengine wakiwa nje ya boksi, Mpanzu alitumia faida ya mwamuzi Ally Mnyupe kuwa bize kufuatilia pigo hilo akazunguka kwa nyuma na kuwahi kuingia ndani.

Chama alipopiga kisha Mgore kuokoa, mpira ukakutana na Mpanzu akaukandamiza nyavuni.

MERIDIANBET WAMELETA MCHEZO WENYE BURUDANI NA MKWANJA FEI TOTO ATESEKA NA MAJERAHA AKING’ARA AZAM