Habari za Simba leo
Simba SC

NGOJA KWANZA….MATOLA ‘ANASEPA’ SIMBA NA HUYU NDIYE MRITHI WAKE…?

admin May 27, 2026 9:41 pm

KOCHA wa Simba, Steve Barker ni kama ameanza kupiga upya hesabu za benchi la ufundi msimu ujao na sasa ametua kwa kocha mmoja aliyezipa shida Yanga na hata Wekundu hao wa Msimbazi msimu huu, akimtaka kwenda kuchukua nafasi ya Seleman Matola anayetajwa kuondoka mwisho wa msimu.

Iko hivi, taarifa za ndani kutoka Simba, zinasema Barker ameukubali uwezo wa Kocha Amani Josiah wa Dodoma Jiji ambaye msimu huu ni kama alikuwa na hesabu dhidi ya Yanga na Simba akizipa mechi ngumu.

Josiah msimu huu ameifunga Yanga akiitibulia rekodi ya kutopoteza mechi ya Ligi Kuu Bara iliyokuwa nayo kwa mechi 42 mfululizo, lakini pia alitangulia kuizuia Simba kushinda ikiwa ugenini ikigawana pointi na Wekundu hao, kabla ya juzi kupoteza kwa bao 1-0.

Barker anamtaka Josiah kwenda kuungana naye kwenye benchi la Simba msimu ujao ambao ni kama anaweza kuwa bila Matola ambaye anapiga hesabu za kuondoka.

Matola anafikiria kuondoka Simba akitajwa kuelekea Geita Gold ambayo ipo karibu kurejea Ligi Kuu Bara na anakwenda kuwa kocha mkuu baada ya kudumu Simba kwa takribani miaka sita akifanya kazi na makocha 10 tofauti wakiwemo tisa wa kigeni na mmoja mzawa, huku yeye akiwa msaidizi.

Habari za Simba LeoKocha huyo aliwahi kufanya kazi Geita Gold ambapo mwaka 2016 ilikuwa ikishiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Inafahamika kuwa Barker amekuwa na mawasiliano ya karibu na Josiah akivutiwa na ufundi aliouweka pale Dodoma Jiji na wawili hao wamekuwa wakiwasiliana vizuri nje ya timu zao kukutana na kupeana changamoto.

“Kocha anatafuta mrithi wa Matola, naona anazungumza sana na Josiah na anakubali sana uwezo wa timu yake, wanazungumza sana mara kwa mara, wakikutana unaona mpira unavyopigwa utasema sio wao ambao wanaongea pamoja,” amesema mmoja wa vigogo wa Simba.

“Matola ni kama anataka kuondoka, kuna timu moja ikipanda tu ligi kuu ataondoka, wanamtaka na anazungumza nao sana, mimi naona ni sawa, bora aende kurudisha ubora wake, unakumbuka kabla alikuwa na timu bora sana.”

Kabla ya kukubali kurudi Simba mwaka 2019 kuwa kocha msaidizi, Matola alizifundisha Lipuli ya Iringa na Polisi Tanzania, ambazo zilikuwa tishio na kutoa upinzani mkubwa, wakati huo zikicheza Ligi Kuu Bara kabla ya Wekundu hao kumbeba kiungo wao huyo wa zamani.

Matola aliyetua Simba mwaka 2019 akitokea Polisi Tanzania, katika miaka saba klabuni hapo akiwa kocha msaidizi, amefanya kazi chini ya makocha 10 tofauti, wakiwamo tisa wa kigeni na mmoja mzawa, huku timu hiyo ikitwaa mataji mawili ya Ligi Kuu Bara, Kombe la Muungano (2) na Kombe la FA na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ilipopoteza kwa RS Berkane ya Morocco kwa jumla ya mabao 3-1.

Habari za Simba leoKwa sasa Geita Gold inaongoza msimamo wa Championship ikiwa na pointi 65 ikifuatiwa na Kagera Sugar (62), zikibaki mechi nne kumaliza msimu huu.

Kwa sasa Geita Gold inahitaji kushinda mechi mbili kati ya nne kufikisha pointi 71 ambazo hazitafikiwa na Mbeya Kwanza wala Polisi Tanzania zilizopo nafasi ya tatu na nne zikikusanya pointi 57 kwani zikishinda zitaishia 69.

MSIKIE JOSIAH

Habari za Simba leoAkizungumzia hilo, Josiah alikiri Barker ni rafiki yake mkubwa na amekuwa akifanya naye mazungumzo ya mara kwa mara kuhusu soka la Afrika Kusini, japo suala la yeye kuhitajika na Simba hana taarifa yoyote.

“Barker ni kocha mzuri sana ambaye tumekuwa na mawasiliano naye ya mara kwa mara kuhusu maendeleo ya soka na jinsi ya kutumia fursa za kujifunza zaidi, kwa sasa hicho ndicho kitu ninachoweza kusema juu ya ukaribu wetu,” amesema Josiah.

Josiah amesema ikiwa kutakuwa na ofa ya kuwa msaidizi wa Barker Simba, ataangalia kama akafanye naye kazi au laa, japo malengo yake kwa sasa yapo kwa waajiri wake Dodoma Jiji ambao ndio alioingia nao makubaliano ya mkataba.

“Mkataba wangu na Dodoma Jiji unafikia tamati mwisho wa msimu huu na hatujaanza mazungumzo mapya, nadhani kwa sasa sio muda sahihi wa kuliangalia hilo kwa sababu tuna mechi tano zimebaki kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho,” amesema Josiah.

Josiah aliyezifundisha timu kadhaa ikiwemo Tunduru Korosho, Biashara United, Geita Gold na Tanzania Prisons, alijiunga na Dodoma Jiji Oktoba 16, 2025, akiwa ni miongoni mwa makocha bora wazawa wanaofanya vizuri kwa sasa.

‘ISHU’ YA IBENGE KUWA KOCHA MKUU MALI….MABOSI AZAM FC WAVUNJA UKIMYA… YANGA, AZAM KUTOANA MACHO KWA MKONGOMANI HUYU…OYA JAMAA SIO POA AISEE..