Simba SC

Simba Yarudi Kwa Kishindo, Taji La CRDB Lachochea Vita Msimu Ujao

Vardo July 5, 2026 8:49 am

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Crescentius Magori, amesema kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB ni uthibitisho kuwa klabu hiyo imerejea kwenye njia ya mafanikio, amesema kuwa kiwango kilichoonyeshwa na kikosi hicho msimu huu kilistahili kuwapa mataji yote mawili ya ndani.

Magori ametoa kauli hiyo baada ya Simba kutwaa taji hilo, akieleza kuwa timu ilionyesha ubora, uthabiti na ushindani mkubwa katika kila mashindano iliyoshiriki kuanzia mwanzo wa msimu hadi mchezo wa fainali.

Amesema, kwa mtazamo wake, Simba ilikuwa na uwezo wa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Kombe la Shirikisho la CRDB, akidai kuwa kama ligi ingeendeshwa kwa haki, timu hiyo ingetwaa mataji yote mawili kutokana na kiwango ilichokionyesha msimu mzima.

“Simba imerejea kwenye njia ya ubingwa.
Tumebeba Kombe la Shirikisho la CRDB, lakini kama ligi ingekuwa ya haki, msimu huu tungebeba makombe yote mawili,” amesema Magori.

Simba imehitimisha msimu wa 2025/26 kwa kutwaa Kombe la Shirikisho la CRDB baada ya kuonyesha kiwango kizuri kuanzia hatua za awali hadi fainali, mafanikio yaliyowapa furaha mashabiki wake na kuongeza matumaini kuelekea msimu wa 2026/27.

Kauli ya Magori imeendelea kuongeza hamasa na joto la ushindani kati ya Simba na Yanga kuelekea msimu mpya, huku kila upande ukijipanga kuwania mataji ya ndani na kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya kimataifa.

Azam Wavunja Ukimya, Sababu Ya Kususia Medali Fainali Kutwaa Ubingwa CRDB, Mpanzu Atuma Onyo Kwa Wapinzani