Simba SC

JKT Tanzania Yamnasa Malimi Baada Ya Kukosa Dili La Simba

Vardo July 16, 2026 5:15 pm

BAADA ya kuwepo kwa taarifa za kipa wa Mtibwa Sugar, Costantine Malimi kuhusishwa na kujiunga na Simba, hatimaye hatma yake imewekwa wazi baada ya JKT Tanzania kufanikiwa kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili. Mkataba huo unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

Awali Malimi alikuwa miongoni mwa makipa waliokuwa kwenye orodha ya kufuatiliwa na Simba SC kwa ajili ya kuimarisha eneo hilo, lakini mipango hiyo haikufanikiwa baada ya kocha mkuu wa Simba, Steve Barker, kutoridhia kuendelea na mchakato wa kumsajili kipa huyo.

Taarifa kutoka ndani ya JKT Tanzania zinaeleza kuwa baada ya Mtibwa Sugar kushuka daraja msimu uliopita, uongozi wa timu hiyo uliamua kutumia nafasi hiyo kumpata Malimi ambaye wanaamini ana uwezo mkubwa na anaweza kuongeza ushindani ndani ya kikosi chao.

Ujio wa Malimi unatarajiwa kuongeza ushindani katika nafasi ya mlinda mlango ndani ya JKT Tanzania, ambapo atakutana na makipa wengine ambao tayari wapo kwenye kikosi hicho akiwemo Omary Gonzo na Ramadhani Chalamanda.

Msimu uliopita Malimi alikuwa miongoni mwa wachezaji walioonyesha kiwango kizuri akiwa na Mtibwa Sugar, huku akimaliza kampeni hiyo akiwa na rekodi ya kuzuia mabao katika baadhi ya michezo na kuonyesha uwezo wa kuisaidia timu yake licha ya changamoto za msimu.

Sasa Malimi anaingia JKT Tanzania akiwa na jukumu la kuwania nafasi ya kwanza langoni, huku akitarajiwa kutoa ushindani kwa Gonzo aliyemaliza na clean sheet nne pamoja na Chalamanda aliyekuwa na clean sheet sita msimu uliopita.

Mwamnyeto Afunguka Yanga, Aacha Sintofahamu Kuhusu Hatma Yake Simba Yaaga nNyota Saba, Yafungua Ukurasa Mpya Kuelekea Msimu Wa 2026/27