Mixx Super App Kutoa Milioni 50 Tamati Ya Kombe La Dunia 2026
Kombe la Dunia 2026: Mixx Super App Kumtangaza Mshindi wa Sh50 Milioni Kampeni Ikielekea Tamati
WAKATI michuano ya Kombe la Dunia ikifikia tamati Jumapili ya Julai 19, 2026, Watanzania wameendelea kunufaika nje ya uwanja kupitia kampeni ya Kombe la Dunia ya “Kila Muamala ni Bao la Ushindi” ambapo washindi 80 tayari wamejishindia fedha taslimu na vifaa vya kisasa vya Hisense.
Kampeni hiyo inayohusisha matumizi ya Mixx Super App kufanya malipo ya huduma mbalimbali za kifedha, imeendelea kuongeza msisimko kwa wateja, huku zawadi zikiendelea kutolewa kila wiki.
Washindi wa Wiki ya Nane Watangazwa
Katika droo ya wiki ya nane iliyofanyika jijini Dar es Salaam, washindi sita wapya walitangazwa:
-
Wanne walikabidhiwa: Fedha taslimu Sh1 milioni kila mmoja.
-
Wawili waliondoka na: Vifaa vya kisasa vya elektroniki kutoka Hisense.
Baadhi ya washindi hao waliotabasamu ni pamoja na Dadi Likuta, Elias Sagiro, John Mkonyi na Ibrahim Mandoa.
Kitita cha Sh50 Milioni Kusaka Mshindi
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Malipo ya Kidijitali wa Mixx, Mshamma Mshamma, amesema mwitikio wa wateja umekuwa mkubwa tuzi tangu kampeni ilipoanza.
“Kampeni hii inazidi kushika kasi na baada ya wiki mbili, tutafanya droo kubwa ambapo mshindi mkuu atazawadiwa Sh50 milioni. Tumekuwa tukitoa zawadi kila siku ambapo washindi wanapata Sh1 milioni na vifaa vya elektroniki kutoka Hisense. Huu ni uwekezaji mkubwa kwa wateja wetu na tunaomba waendelee kushiriki,” amesema Mshamma.
Lengo kuu la kampeni hii kupitia Mixx Super App ni kurahisisha huduma za kifedha nchini na wakati huo huo kurudisha fadhila kwa kuwazawadia watumiaji wake waaminifu.
Ushuhuda wa Washindi
Mmoja wa washindi wa wiki hii, Ibrahim Mandoa kutoka Kinondoni, ameeleza furaha yake na kuthibitisha kuwa kampeni hiyo ni ya kweli na ya uwazi.
“Sikutegemea kabisa kushinda, lakini leo nimejionea mwenyewe. Ninawahimiza Watanzania wenzangu kutumia Mixx Super App kufanya malipo yao kwa sababu nafasi ya kushinda ipo wazi kwa kila mtumiaji,” amesema Mandoa.
Jinsi ya Kushiriki
Muda bado upo! Ili kuingia kwenye droo inayofuata na kuwa kwenye nafasi ya kunyakua zawadi kuu ya Sh50 milioni, unachotakiwa kufanya ni kuendelea kufanya malipo ya huduma mbalimbali za kijamii na kifedha kupitia programu ya Mixx Super App.