Selemani Mwalimu Simba SC
Simba SC

Selemani Mwalimu ARejea Simba SC: Azani Kurejea Msimu wa 2026/27

Vardo August 8, 2026 7:26 pm

DAR ES SALAAM, Tanzania — Klabu ya Simba SC imekamilisha rasmi mchakato wa usajili wa mshambuliaji wao hatari, Selemani Mwalimu, akitokea miamba ya soka nchini Morocco, Wydad AC. Mchezaji huyo tayari yupo safarini kurejea nchini kujiunga na kikosi cha Wekundu wa Msimbazi tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa mashindano wa 2026/27.

Mwalimu, ambaye alikuwa akicheza Simba kwa mkopo msimu uliopita, amefanikiwa kuuteka moyo wa uongozi wa Simba kutokana na kiwango chake bora cha kufumania nyavu, jambo lililofanya mabosi wa Msimbazi kupambana kufa na kupona ili kupata saini yake ya kudumu.

Ahmed Ally Athibitisha Mambo Yote Kukiwaka

Akizungumza baada ya kutambulishwa kwa kikosi kitakachopambana msimu ujao, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, alisema mchakato wa kumpata Mwalimu haukuwa mwepesi.

“Kuna mambo mengi yalitokea na jitihada nyingi zilifanyika ili mradi tu tumkose mshambuliaji huyu. Lakini kwa juhudi na ukukazania wa viongozi wetu, tumefanikiwa kumpata Mwalimu na hivi sasa yupo angani akirejea nchini kujiunga na familia ya Simba,” alisema Ahmed Ally.

Kurejea kwa Selemani Mwalimu kunatajwa kuwa silaha kubwa katika safu ya ushambuliaji ya Simba SC, inayojiandaa kusaka mataji ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).


Tazama Kikosi Kamili Cha Simba SC Msimu wa 2026/27

Mbali na Mwalimu, Mabingwa hawa wa Kombe la Shirikisho la CRDB wametambulisha majina ya wachezaji watakaovaa jezi ya Wekundu wa Msimbazi msimu huu:

Makipa (Goalkeepers):

  • Erasto Alex

  • Hussein Abel

  • Djibrilla Kasali

  • Yakubu Selemani

Mabeki (Defenders):

  • Bashiru Kibaila, David Kameta, Dedastus Masinde, Nathaniel Chilambo

  • Anthony Mligo, Ismail Toure, Wilson Nangua, Hussein Mbegu

  • Abdulrazak Hamza, Nickson Kibabage, Rusheine De Ruuck na Shomari Kapombe

Viungo (Midfielders):

  • Yusuph Kagoma, Neo Maema, Morice Abraham

  • Inno Loemba, Kelvin Nashon na Hussein Semfuko

Washambuliaji (Forwards):

  • Libasse Gueye, Bakari Msimu, Keletso Makgalwa, Anicet Oura

  • Ibrahim Jabaar, Elie Mpanzu, Clatous Chama, Ibrahim Doumbia na Selemani Mwalimu

Kurejea kwa Mwalimu kunaongeza hamasa na ushindani mkubwa katika kikosi cha Simba SC huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona safu hiyo ya ushambuliaji ikianza kazi kwenye msimu mpya!

Simba Queens Yaitambulisha Safu Mpya Simba Day: Mgosi Aongoza Jahazi! Mo Dewji Wazi: Aweka Mezani Bilioni 30 Kuisuka Simba Upya