Yanga Day 2026
Yanga SC

Yanga Day 2026: Kilele Kufanyika Uhuru, Shalulile na Kangwanda Waahidi Makubwa

Vardo August 9, 2026 10:12 am

DAR ES SALAAM, Tanzania — KILELE cha tamasha kubwa la Yanga Day 2026 kinatarajiwa kutimua vumbi leo Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, kikihitimishwa kwa mechi kabambe ya kirafiki ya kimataifa kati ya mabingwa hao wa nchi, Yanga SC, dhidi ya Les Aigles Du Congo.

Tamasha la mwaka huu linawandikisha historia kwani ni mara ya nane mfululizo kufanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2019. Klabu ya Yanga imekuwa ikilitumia tamasha hili la aina yake kutoa burudani kabambe kwa mashabiki wake pamoja na kutambulisha rasmi kikosi kamili cha msimu mpya na benchi zima la ufundi.

Ally Kamwe: Milango Kufunguliwa Mapema, Burudani ni Mwanzo Mwisho

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, amethibitisha kuwa maandalizi yote yamekamilika na wamejipanga kutoa burudani ya kipekee itakayowekwa kama mfano wa kuigwa.

“Tukifungua mageti tu, burudani inaanza moja kwa moja. Kama kuna msimu ambao tumetamani kukata kiu ya wanachama wetu kwa kiwango cha juu ni msimu huu wa Yanga Day. Tunataka tamasha la mwaka huu liwe la mfano wa kuigwa,” alisema Kamwe.

Kamwe aliongeza kuwa milango ya Uwanja wa Uhuru itakuwa wazi kuanzia saa 5:00 asubuhi ili kuwezesha mashabiki, wanachama na ‘Wananchi’ wote kuingia kwa utulivu na kuanza kufurahia shughuli hiyo mapema.

Shalulile, Okello na Kangwanda Kushiriki kwa Mara ya Kwanza

Upande wa wachezaji nao haujabaki nyuma, kwani nyota wapya wa timu hiyo wameahidi kutoa burudani ya kiwango cha juu uwanjani.

Mshambuliaji mpya wa timu hiyo kutoka Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Peter Shalulile, amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi: “Njooni mfurahie Yanga Day na muwe na wakati mzuri wa pamoja.”

Kwingineko, winga raia wa Uganda, Allan Okello, aliyejiunga na Yanga dirisha dogo, alieleza furaha yake ya kushiriki tukio hili kwa mara ya kwanza: “Kwangu mimi itakuwa ni mara yangu ya kwanza kushiriki shughuli hii kubwa ya Yanga Day na nina furaha tele kuwepo hapa.”

Naye nyota mpya raia wa Zambia, Albert Kangwanda, aliongeza kuwa ana msisimko mkubwa wa kucheza mbele ya mashabiki wa Yanga: “Njooni kwa wingi kutusapoti. Nimekuwa nikitazama tamasha hili kwa muda mrefu na msimu huu nina msisimko mkubwa kuwa sehemu yake.”

Simba Day 2026: Simba Yachapwa 1-0 na Kenya Police Uwanja wa Uhuru Chipukizi FC Yafanya Kufuru: Yashusha Mashine 6 Mpya na Kocha Mpya Ligi Kuu Zanzibar 2026/2027