Yanga vs Pamba Jiji
Yanga SC

Kamwe Atoa Onyo Uzito: Yanga vs Pamba Jiji KMC Complex Kesho, Awaomba Mashabiki Hili

Vardo August 27, 2026 9:42 am

Klabu ya Yanga kesho Ijumaa inatarajiwa kushuka uwanjani kwenye mechi nyingine kali ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Pamba Jiji, mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa KMC Complex, Mwenge.

Akizungumzia mchezo huo, Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi ili kuwapa morali wachezaji wao na kuendeleza msururu wa matokeo mazuri.

Kamwe ameonya kuwa ingawa Pamba Jiji haijaanza msimu vizuri, bado ni timu hatari inayoweza kushtua wengi uwanjani, hivyo Yanga haipaswi kuingia kwa kujiamini kupita kiasi.

“Mchezo dhidi ya Pamba Jiji ni dhidi ya timu ambayo haijaanza vizuri, lakini ina uwezo wa kuja kupambana na kutoa matokeo ya kushtukiza—jambo ambalo hakuna Mwanayanga anayetamani litokee,” amesema Kamwe.

Amesisitiza kuwa mahudhurio ya mashabiki bado yanahitaji kuongezeka zaidi hadi uwanja ujae kabisa.

Mipango ya Shangwe Uwanjani

Ili kunogesha mechi hiyo, uongozi wa Yanga unaendelea kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya mashabiki.

Eneo la chini lililojengwa kwa sakafu chini ya majukwaa limepangwa kutumika kama sehemu maalumu ya mashabiki kuruka na kushangilia wakati mechi ikiendelea.

Kamwe amehitimisha kwa kusema maandalizi ya kikao hicho yanakwenda vizuri na uwepo wa mashabiki wengi utakuwa chachu ya ushindi kwa timu hiyo.

Pigo Kubwa Simba SC: Nickson Kibabage Nje Wiki 4, Akosa Mechi Zote Hizi Za Moto! Simba SC vs Coastal Union Leo: Mshikemshike wa Ligi Kuu Kuroga Mbweni!