Ligi Kuu Zanzibar 2026-2027
Michezo Bongo

Kocha Black Sailors Aweka Wazi Mkakati wa Kutisha Ligi Kuu Zanzibar 2026/27

Vardo August 28, 2026 6:37 pm

KOCHA Mkuu wa Black Sailors, Mohammed Ali Hilal ‘Tedy’, ameweka wazi kuwa lengo lao kuu kwa sasa ni kuanza kwa kishindo msimu mpya wa Ligi Kuu Zanzibar 2026-2027 kwa kuhakikisha wanavuna matokeo chanya katika michezo yao minne ya kwanza.

Tedy ameeleza kuwa maandalizi ya kikosi hicho yanakwenda vizuri na yanaimarika siku hadi siku mazoezini. Wachezaji wote wameonyesha utayari mkubwa wa kufanyia kazi mbinu za kiufundi na kiushindani kabla ya msimu rasmi kung’oa nanga.

Akizungumza kuhusu mikakati hiyo, Kocha Tedy amesisitiza umuhimu wa kuanza vizuri ili kujenga mwelekeo wa msimu mzima.

“Mechi nne za mwanzo ni muhimu sana kwa timu kujenga mwelekeo mzuri. Hivyo basi, tunahitaji kuwa umakini wa hali ya juu na kutumia vyema kila nafasi tutakayopata ili kupata ushindi,” alisema Tedy.

Pamoja na hayo, benchi la ufundi linaendelea kujenga mshikamano na hali ya kujiamini kikosini, huku kila mchezaji akitakiwa kutimiza majukumu yake kwa asilimia 100 ndani ya mfumo wa timu.

Ratiba ya Mechi 4 za Kwanza za Black Sailors (Ligi Kuu Zanzibar 2026/27):

  • Agosti 31, 2026: Black Sailors vs Chipukizi United (Mchezo wa kwanza nyumbani baada ya kupanda daraja)

  • Septemba 3, 2026: Black Sailors vs Wembe

  • Septemba 12, 2026: Black Sailors vs FSC

  • Septemba 16, 2026: Black Sailors vs Mwenge

Mashabiki Simba Mbeya Waandaa Coaster 5 Kuivamia Mighty Wanderers Malawi Suleiman Kidawa Aweka Wazi Sababu za Kurejea Ligi Kuu Zanzibar, Aingia KVZ