Simba SC vs Mighty Wanderers
Michezo Bongo

Mashabiki Simba Mbeya Waandaa Coaster 5 Kuivamia Mighty Wanderers Malawi

Vardo August 28, 2026 6:28 pm

MBEYA: Wakati Simba SC ikiendelea na maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold utakaochezwa Agosti 31, 2026, mashabiki wa klabu hiyo jijini Mbeya wameanza mikakati mizito ya kuivamia Mighty Wanderers nchini Malawi kwenye mchezo wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).

Baada ya kukamilisha ratiba ya ndani dhidi ya Geita Gold, Wekundu wa Msimbazi watasafiri kuelekea Lilongwe, Malawi kujaribu bahati yao Septemba 6, 2026 katika Uwanja wa Bingu.

Simba wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu nzuri nchini humo, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Nyasa Big Bullets Septemba 10, 2022 katika uwanja huo huo wa Bingu, huku Moses Phiri akipachika mabao yote mawili.

Hamasa Ya Mashabiki Mbeya

Simba imeanza msimu wa 2026-2027 kwa kasi ya ajabu ikishinda mechi nne mfululizo za Ligi Kuu:

  • Kagera Sugar: 2-0

  • Pamba Jiji: 2-1

  • Singida Black Stars: 2-1

  • Coastal Union: 1-0

Kasi hii imeongeza hamasa kubwa kwa mashabiki. Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Simba Mkoa wa Mbeya, Yusuph Mwandete, amethibitisha kuwa wameandaa usafiri wa Coaster tano zitakazobeba jumla ya mashabiki 150 kwenda kutoa sapoti ya nguvu nchini Malawi.

“Hatuendi kwa historia pekee, bali kwa ubora wa kikosi chetu na mipango thabiti tuliyo nayo msimu huu. Tunaimani tutashinda na kuanza vyema kampeni ya kuisaka fainali ya klabu bingwa,” amesema Mwandete.

Shabiki mwingine wa timu hiyo, Benjamin James, amesisitiza kuwa kikosi cha msimu huu kinategemea ushirikiano wa timu nzima badala ya staa mmoja mmoja, na amewasihi wachezaji kutowachukulia poa mabingwa hao wa Malawi.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kupigwa Septemba 11, 2026 jijini Dar es Salaam, ambapo mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya 15 De Agosto au Fomboni kuwania nafasi ya kutinga hatua ya makundi.

Hamisa Mobetto Afunguka Siri ya Ndoa Yake na Aziz KI, Ubalozi UNESCO na Ng’ombe 30 za Mahari Kocha Black Sailors Aweka Wazi Mkakati wa Kutisha Ligi Kuu Zanzibar 2026/27