Wachezaji EPL 2026/27
Habari za michezo

Wachezaji 6 EPL Wanaorejea kwa Kasi Msimu wa 2026/27

Vardo August 29, 2026 10:04 am

LONDON, ENGLAND: Maisha katika ligi kuu za soka barani Ulaya yameshaanza upya, na kila timu ipo kwenye vita kali ya kuwania ufalme. Baada ya kupitia kipindi kigumu msimu uliopita kutokana na majeraha, kuporomoka kwa viwango au changamoto za kiumri, baadhi ya wachezaji mafundi wa Ligi Kuu England (EPL) wameanza msimu wa 2026/27 kwa kasi kubwa wakilenga kurejesha ubora wao wa zamani.

Mechi za kwanza za msimu tayari zimeonyesha picha ya awali ya kile kinachokuja. Hawa hapa ni miongoni mwa nyota wanaolenga kuwasahaulisha mashabiki machungu ya msimu uliopita:

1. Cole Palmer (Chelsea) Cole Palmer alihitaji sekunde 31 tu katika mchezo wa kwanza wa msimu kufikisha idadi ya pasi za mabao alizotoa msimu mzima uliopita. Mpira wake wa mapema dhidi ya Fulham ulimaliziwa na Joao Pedro, kabla ya Palmer mwenyewe kufunga bao la ushindi.

Baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha England kilichoshiriki Kombe la Dunia 2026 chini ya Thomas Tuchel, mapumziko ya kiangazi yameonekana kumrejeshea utimamu wa mwili na kiwango kilichomfanya ahusike kwenye mabao 56 katika misimu yake miwili ya kwanza Stamford Bridge.

2. Martin Odegaard (Arsenal) Nahodha wa Arsenal, Martin Odegaard, alicheza asilimia 35 tu ya dakika zote za msimu uliopita kutokana na majeraha ya mara kwa mara. Hata hivyo, kiwango chake bora akiwa na Norway kwenye Kombe la Dunia 2026 kiliashiria kurejea kwa fundi huyo.

Katika ushindi wa mabao 3-0 wa Arsenal kwenye mechi ya kwanza ya msimu, Odegaard aliongoza safu ya ushambuliaji kwa pasi za hatari akishirikiana vyema na Bukayo Saka na Ben White. Tayari amefunga mabao mawili msimu huu (ikiwemo la Ngao ya Jamii), akivuka idadi ya bao moja alilofunga msimu mzima uliopita.

3. Anthony Elanga (Newcastle United) Tangu ahamie Newcastle United kutoka Nottingham Forest kwa ada ya Pauni milioni 55, Elanga alipitia wakati mgumu akicheza mechi 32 bila kufunga bao hata moja msimu uliopita.

Hata hivyo, mbio zake zenye kasi ya kilomita 34.9 kwa saa dhidi ya Liverpool zilimwezesha kufunga bao lake la kwanza la ligi akiwa na Newcastle, akimaliza ukame wa mechi 40 bila kufunga. Kasi yake na uwezo wa Newcastle kucheza mashambulizi ya kushtukiza vinaweza kumfanya Elanga kuwa tishio kubwa zaidi msimu huu.

Vita ya Pointi Tisa! Raundi ya Ligi Kuu Bara Kuunguruma Leo Jumamosi Vita Ya Fainali CECAFA Women 2026: Kawempe Yaisaka CBE, Police Bullets Kuikabili Yei