Usajili wa Mpira Ulaya
Michezo

Liverpool Yaiwazia Tena Sarr Januari, Richarlison Kuelekea Saudia & Habari Nyingine za Usajili

Vardo September 6, 2026 5:17 pm

Klabu ya Liverpool inatarajiwa kurejea tena mezani mwezi Januari kujaribu kumsajili winga wa Crystal Palace, Ismaila Sarr, baada ya dili hilo kukwama katika siku za mwisho za dirisha la usajili lililopita.

Liverpool ilikuwa ikimfuatilia kwa karibu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, lakini Crystal Palace ilikataa kutoa ruhusa kwa raia huyo wa Senegal kuondoka Selhurst Park. Licha ya Sarr kuonyesha nia ya kujiunga na miamba hiyo ya Anfield, ilimbidi kubaki klabuni hapo.

Kocha wa Crystal Palace, Pierre Sage, ameeleza kuwa Sarr anahitaji muda wa kutulia baada ya usajili huo kufeli, huku akisisitiza kuwa bado ni mchezaji muhimu kwenye mipango ya timu hiyo msimu huu. Mbali na Sarr, Liverpool pia ilikuwa ikimfuatilia winga wa Brighton, Yankuba Minteh.


Yajue Mengine Yaliyojiri kwenye Soko la Usajili:

  • Richarlison Kuelekea Saudi Arabia: Mshambuliaji wa Tottenham, Richarlison (29), yuko kwenye mazungumzo ya kuhamia Ligi Kuu ya Saudi Arabia (Saudi Pro League) baada ya usajili wake kwenda Trabzonspor kufeli.

  • Mikel Arteta Kubaki Arsenal: Arsenal iko hatua za mwisho kukamilisha mkataba mpya na kocha Mikel Arteta. Pia, klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo ya kuwaongezea mikataba Declan Rice, Martin Odegaard, na Jurrien Timber.

  • Man United Bado Inamtaka Lewis Hall: Manchester United inaendelea kumfuatilia beki wa kushoto wa Newcastle United, Lewis Hall (21), ikipanga kumng’oa majira ya joto yajayo.

  • Amadou Onana Aongeza Mkataba Villa: Kiungo Amadou Onana amesaini mkataba mpya wa miaka miwili unaombakiza Aston Villa hadi mwaka 2031.

  • AC Milan Haichoki kwa Goncalo Inacio: AC Milan inajipanga kuwasilisha ofa mpya mwezi Januari ili kumsajili beki wa Sporting Lisbon, Goncalo Inacio (25).

  • Louis Page Kutua Old Trafford? Manchester United inaendelea na mazungumzo na Leicester City kwa ajili ya kumsajili kiungo kijana Louis Page (18).

  • Karim Benzema Kukwama Lyon: Mpango wa Karim Benzema (38) kurejea Lyon umekwama kutokana na makubaliano yake ya ubalozi wa Saudi Pro League yanayomfunga hadi mwaka 2030.

  • Lens Yamwekea Ngumu Udol: Aston Villa na Sunderland zilifanya jitihada za kumsajili beki Matthieu Udol (30), lakini klabu yake ya Lens ilikataa kumuuza.

  • Arsenal Yagonga Mwamba kwa Schade: Arsenal iliulizia uwezekano wa kumsajili winga Kevin Schade (24), lakini Brentford ilifunga milango ya kumuuza.

Lisa Baum Aanza Na Bao Arsenal Dhidi Ya Brighton WSL Ronaldo na Messi Kucheza Timu Moja? Carlos Tevez Aandaa Mchezo wa Aina Yake La Bombonera