Neo Maema Simba vs Mighty Wanderers
Simba SC

Maema Aichana Simba, Aionya Mighty Wanderers Ligi ya Mabingwa Afrika

Vardo September 6, 2026 9:55 am

KIUNGO mshambuliaji wa Simba SC, Neo Maema, amesisitiza kuwa hawatabweteka wala kuwachukulia poa wenyeji wao, Mighty Wanderers ya Malawi, katika mchezo wa leo wa raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).

Simba inashuka dimbani leo nchini Malawi ikilenga kupata matokeo chanya ugenini kabla ya kurejea Dar es Salaam kwa mchezo wa marudiano.

“Wanderers Si Timu ya Kubeza”

Maema amebainisha kuwa Simba inatambua vyema ubora wa Mighty Wanderers, huku akitolea mfano rekodi yao ya kuvutia katika ligi ya ndani ya Malawi msimu uliopita ambapo walipoteza mchezo mmoja pekee.

“Ni mchezo ambao utakuwa mgumu sana. Tunacheza na timu ambayo msimu uliopita ilipoteza mchezo mmoja tu katika ligi yao ya ndani. Wanacheza nyumbani, hivyo tunajua watakuwa na hamasa kubwa,” alisema Maema.

Morali ya Wachezaji Iko Juu

Pamoja na kukiri ugumu wa pambano hilo, Maema ameeleza kuwa kikosi cha Simba kiko kwenye hali nzuri ya kisaikolojia baada ya kupata mfululizo wa matokeo mazuri hivi karibuni.

Amesema wachezaji wameungana na kuwa kitu kimoja baada ya kupitia changamoto mbalimbali, na sasa lengo kubwa ni kuendeleza furaha hiyo uwanjani.

“Hakuna Timu Rahisi CAF”

Kiungo huyo aliongeza kuwa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika yanazikutanisha timu bora pekee, hivyo hakuna nafasi ya kufanya makosa au kumdharau mpinzani.

“Ligi ya Mabingwa haina timu rahisi. Kila timu iliyofika hapa ni bingwa au ipo kileleni kwenye ligi yake. Inatupasa kuwa makini na wenye weledi kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho ili kupata matokeo tunayoyataka kwa ajili ya klabu na mashabiki wetu,” alisisitiza.

Kupambana Hadi Dakika ya Mwisho

Maema alimalizia kwa kusema kuwa kocha mkuu, Steve Berker, amekuwa akiwasisitizia umuhimu wa kuwa na nidhamu ya mchezo na kupambana bila kukata tamaa hata pale mchezo unapokuwa mgumu.

Juana Ortegon: Nahodha wa Colombia Atangaza Vita Kombe la Dunia U-20 Steve Barker Aitahadharisha Mighty Wanderers: Simba Tuko Tayari Ligi ya Mabingwa!