Q Chief kuimba live
Burudani

Q Chief: Hakuna Wa Kumfunika Kuimba Live Tanzania, Hata Diamond au Alikiba

Vardo September 7, 2026 8:54 am

HAKUNA WA KUMFUNIKA! Ndivyo anavyojiamini msanii mkongwe na maarufu wa Bongo Fleva, Abubakary Katwira ‘Q Chief’, anapozungumzia uwezo wake mkubwa wa kuimba moja kwa moja (live performance).

Q Chief ameweka wazi kuwa amefikia kiwango cha juu sana cha uimbaji kiasi kwamba haoni msanii mwingine yeyote nchini anayeweza kumzidi kwenye jukwaa la live band, akiwamo mastaa wakubwa kama Diamond Platnumz na Alikiba.

Akizungumza hivi karibuni maeneo ya Sinza kwa Remmy, mkali huyo alieleza kuwa kumfananisha au kumweka kwenye vipimo na msanii mmoja mmoja ni sawa na kumshushia daraja lake la muziki.

“Sasa hivi nilipofikia, mpango wa kunitajia msanii mmoja mmoja kwamba atanifunika ni kunishusha daraja na thamani yangu. Chukua Diamond, Alikiba, Marioo, Jay Melody — wakiweza kunifunika kwenye kuimba live, ndipo nitaamini kweli Tanzania kuna wasanii,” alisema Q Chief.

Msanii huyo aliongeza kuwa kujiamini huko kupitiliza hakutokana na majivuno, bali ni kipaji halisi alichojaliwa na Mwenyezi Mungu ambacho hakihitaji kulazimishwa.

Ingawa Diamond, Alikiba, Marioo na Jay Melody wanaweza kuwa na majina makubwa pamoja na mashabiki wengi kwa sasa, Q Chief anasisitiza kuwa linapokuja suala la kusimama jukwaani na kuimba live, bado hajapatikana wa kushikana naye shati nchini Tanzania.

Azam FC vs Namungo FC Leo: Kipimo cha Ibenge na Mgunda Ligi Kuu Cyprian Kachwele Ajiunga na Kryvbas ya Ukraine Kwa Mkataba wa Miaka 4