Simba vs Mighty Wanderers
Simba SC

Simba SC vs Mighty Wanderers: Jabaar Afunguka Mchezo wa Marudiano CAFCL

Vardo September 8, 2026 5:47 pm

Mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League) kati ya Simba SC na Mighty Wanderers ya Malawi unatarajiwa kuwa wa vuta-nikuvute, huku kiungo nyota wa Simba, Ibraheem Jabaar, akithibitisha kuwa hatua inayofuata ipo mikononi mwa wachezaji wenyewe.

Simba SC imerejea nchini ikitokea Malawi ikiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 ugenini. Hata hivyo, Jabaar amebainisha kuwa matokeo hayo hayawafanyi wabweteke, bali yanawapa hamasa ya kupambana zaidi katika dakika 90 zijazo.

Kazi Bado Haijamalizika Akizungumzia mchezo huo utakaopigwa Septemba 13 kwenye Uwanja wa Uhuru, Jabaar raia wa Nigeria alisema:

“Tulikuwa ugenini kwenye mchezo uliopita na lengo kuu lilikuwa kupata pointi tatu. Hata kama hatukucheza kwa kiwango chetu cha juu zaidi, tulifanikiwa kupata ushindi muhimu. Lakini bado hatujamaliza kazi.”

Kuwafurahisha Mashabiki Nyumbani Jabaar aliongeza kuwa kucheza mbele ya mashabiki wa nyumbani kunawapa jukumu kubwa la kudhihirisha ubora wao kwa kucheza soka la kuvutia na kupata ushindi mnono zaidi.

“Tunaporudi nyumbani, jukumu la kuamua mchezo linabaki kwetu wachezaji. Tutakuwa mbele ya mashabiki wetu, hivyo tuna nafasi kubwa ya kuwapa burudani na matokeo mazuri wanayostahili.”

Kikosi Kinaendelea Kuimarika Tangu asajiliwe akitokea Stellenbosch ya Afrika Kusini, Jabaar amekuwa nguzo muhimu kwenye safu ya kiungo ya Wekundu wa Msimbazi. Amebainisha kuridhishwa na namna kikosi kinavyozidi kuungana na kujenga ushirikiano imara kila mechi.

Licha ya kutomiliki mpira kwa kiasi kikubwa ugenini, ulinzi imara wa Simba uliwezesha timu hiyo kutoka bila kuruhusu bao (clean sheet), jambo analoliona kama msingi mzuri wa mafanikio kuelekea mchezo wa marudiano.

Chama Azungumzia Mechi ya Marudiano Simba vs Mighty Wanderers CAF Champions League