Riyama Ally na Leo Mysterio
Burudani

Riyama Ally Afunguka Nzito Kuhusu Kutengana na Leo Mysterio: “Hatuachani Ng’o!”

Vardo September 11, 2026 8:19 am

Staa mahiri wa filamu nchini Tanzania, Riyama Ally, ameibuka na kuvunja ukimya kufuatia taarifa zinazoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai ametengana na mume wake, Leo Mysterio.

Mwanamuziki na mwigizaji huyo ametoa msimamo wake baada ya kuonekana tena wakiwa pamoja hivi karibuni, jambo lililowapa majibu majibu wale wote waliokuwa wakisambaza tetesi za kuvunjika kwa ndoa yao.

Wawili hao waliingia kwenye ahadi ya ndoa Juni 16, 2016, na hivi karibuni wametimiza miaka 10 ya ndoa yao—safari ambayo imekuwa ikigubikwa na maneno ya kila namna kutoka kwa mashabiki na wakosoaji.

Akizungumza kwa utulivu kuhusu uvumi huo, Riyama alibainisha kuwa ameshazoea tabia ya watu kuzungumzia maisha yake ya kibinafsi bila kuwa na ukweli wowote, na kwamba hana mpango wa kutumia muda wake kujibu kila kinachosemwa.

“Watu wakiamua kusema lao wanasema bila kuwa na uhakika wa jambo. Hivyo wakiwa wanasema mimi huwa naangalia tu, kwani sina muda wa kujibizana nao kuhusu maisha ya ndoa yangu,” alisema Riyama.

Sababu za Ndoa ya Riyama Ally Kudumu Miaka 10:

  • Kupuuza Maneno ya Watu: Wawili hao wamechagua kuangazia mapenzi na familia yao badala ya kusikiliza maoni ya mitandaoni.

  • Kuheshimiana na Kuvumiliana: Riyama ameweka wazi kuwa siri ya kukaa pamoja kwa miaka yote hiyo ni misingi ya heshima na uvumilivu.

  • Kutoweka Maisha Binfasi Hadharani: Wanandoa hao wameamua kuishi maisha yao kwa misingi yao wenyewe bila kuweka presha ya kujieleza kwa umma.

Kauli hii mpya inazima rasmi uvumi wa kuachana kwao, huku Riyama akionekana kuendelea na maisha yake kwa amani na furaha tele pembeni mwa mume wake Leo Mysterio.

Mchakato wa Jezi Mpya Taifa Stars AFCON Unatakiwa Anza Sasa Dodoma Jiji vs Namungo FC: Vita ya Pointi 3 Usiku wa Leo Ligi Kuu