Jezi Mpya Taifa Stars AFCON
Michezo Bongo

Mchakato wa Jezi Mpya Taifa Stars AFCON Unatakiwa Anza Sasa

Vardo September 11, 2026 8:12 am

KUNATAKIWA uwepo wa jezi mpya za Taifa Stars kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) zitakazofanyika hapa nchini, na uzinduzi wake unatakiwa ufanyike mapema mwaka huu.

Leo tukiwa katika mwezi wa tisa, zimebaki miezi michache tu mwaka huu umalizike kabla ya kuingia mwakani ambapo mashindano hayo makubwa yatafanyika yakiandaliwa na Tanzania ikishirikiana na majirani zetu wa Kenya na Uganda (EA Pamoja).

Imebaki takribani miezi nane kabla ya kuanza kwa mashindano hayo kwa mara ya kwanza katika ardhi ya nchi yetu—jambo ambalo ni historia kubwa na ya kipekee kwa soka la Kitanzania.

Wakati wadau na mashabiki wakijipanga kwa ajili ya mashindano haya, kitengo kinachohusika na vifaa vya timu ya taifa kinatakiwa kufanya mpango wa kuleta toleo jipya la jezi za Taifa Stars badala ya zile zinazotumika sasa. Jezi za hivi sasa zilizinduliwa muda mrefu sana na zimetumika kwenye mechi nyingi mfululizo bila kuwepo kwa mabadiliko kama wanavyofanya mataifa mengine makubwa duniani.

Jezi zitakazotumiwa na Taifa Stars kwenye AFCON hazitakiwi kuwa za ‘bora liende’ au kubahatisha kwa sababu tu watu wana hamasa na watazinunua. Zinatakiwa kubuniwa kwa kiwango cha juu sana ambacho kitawavutia mashabiki kuzivaa kwa pride, huku zikibeba utamaduni, maana, na thamani halisi ya Taifa Stars.

Ikiwa wahusika wanaona ubunifu wa ndani ni changamoto, ni vyema ukaanzishwa mchakato au shindano maalum la kutoa fursa kwa wabunifu wa kitanzania kuwasilisha sampuli zao, kisha mshindi apatikane kwa njia ya uwazi.

Kila mmoja anatakiwa kuunga mkono maandalizi ya AFCON kwa kutimiza wajibu wake mapema—na kwa kuanzia, TFF na wabunifu wa jezi lazima watupe kitu cha tofauti mapema kabisa!

Fei Toto Agoma Kuzungumzia Yanga na Simba, Aweka Wazi Mkataba Wake Azam FC Riyama Ally Afunguka Nzito Kuhusu Kutengana na Leo Mysterio: “Hatuachani Ng’o!”