AFCON 2027 Tanzania
Michezo

AFCON 2027: Serikali Yatoa Sh104 Bilioni Haki za Matangazo na Uenyeji – Makonda

Vardo September 24, 2026 12:52 pm

Serikali ya Tanzania imeweka wazi kuwa imeshalipa jumla ya Shilingi 104 bilioni kwa ajili ya maandalizi na kupata haki ya matangazo ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027).

Taarifa hiyo imetolewa leo, Septemba 24, 2026, na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kuzungumzia maandalizi ya mashindano hayo makubwa ya soka barani Afrika, mashindano ya Miss World, pamoja na mfumo wa ugawaji wa mirabaha kwa wasanii.

Akimchambua mchanganuo wa fedha hizo, Makonda alieleza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha nafasi hii ya pekee inatumiwa kimkakati zaidi ya michezo ili kuitangaza Tanzania duniani kote.

“Serikali imelipa shilingi 74 bilioni pesa ya kuwa mwenyeji tu wa mashindano ya AFCON. Bilioni 30 kwa ajili ya kupata haki ya matangazo, kama nchi tumelipa fedha hizo ili tupate uhalali na waone sehemu sahihi,” alisema Makonda.

Waziri Makonda aliongeza kuwa mashindano haya ya AFCON 2027 yatakuwa chachu kubwa ya kukuza uchumi na kufungua fursa mpya za ajira kwa vijana. Serikali inalenga kutumia ujio wa wageni na mashabiki wa soka kutoka pande zote za dunia kuonyesha fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini.

“Ili watakaokuja waone Tanzania, waone sehemu sahihi ya kuwekeza na vijana wapate ajira,” alisisitiza.

Tanzania itakuwa mwenyeji mwenza wa Fainali za AFCON 2027 ikishirikiana na nchi jirani za Kenya na Uganda, hatua inayotajwa kuwa ya kihistoria kwa ukanda wa Afrika Mashariki (EAF).

Makonda Atoa Neno Zito kwa ‘Content Creators’, Awapa Michongo ya Sh2 Bilioni! Maandalizi ya AFCON 2027: Serikali Yatoa Kauli Nzito Kuelekea Desemba 2026