Ngorongoro Heroes vs Sudan U20
Michezo

Ngorongoro Heroes Yaangukia Pua Fainali CECAFA U20 Mbele ya Sudan

Vardo September 25, 2026 10:28 am

TIMU ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 ya Tanzania, Ngorongoro Heroes, imeshindwa kutetea ubingwa wake wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA U-20) baada ya kukubali kichapo cha penalti 4-3 dhidi ya Sudan katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mchezo huo wa vuta-nikuvute ulikamilika kwa sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 120 kabla ya kuamuliwa kwa matuta.

Ngorongoro Heroes, ambao waliaza michuano hiyo wakiwa mabingwa watetezi wa mwaka 2024, walikutana na wakati mgumu baada ya Sudan kupata bao la kuongoza katika dakika ya 93 kupitia kwa Omer Hamdi.

Hata hivyo, wachezaji wa akiba wa Tanzania walibadilisha upepo wa mchezo ambapo Abdulnasir Abdallah ‘Casemiro’ alisaawazisha bao hilo katika dakika ya 113 akimalizia pasi safi kutoka kwa Farid Mzalendo.

Tanzania na Sudan Zatikisa Kwenye Njia ya AFCON U20

Pamoja na matokeo hayo ya fainali, timu zote mbili tayari zilikuwa zimeshakata tiketi ya kushiriki Fainali za AFCON U-20 zitakazofanyika nchini Ghana mwaka 2027 baada ya kufanya vizuri katika hatua ya nusu fainali.

Tanzania iliingia fainali ikiwa na rekodi ya kuvutia ya kushinda mechi zake zote tatu za makundi bila kuruhusu bao lolote na ikiwa imefunga mabao 9, huku Sudan ikiwa imetupia mabao sita.

Mbinu za Makocha na Soka la Tahadhari

Kocha wa Ngorongoro Heroes, Mario Rivera Campesino, pamoja na Kocha wa Sudan, Salaheldin Ahmed, waliamua kucheza kwa tahadhari kubwa ili kuzuia makosa.

Tofauti na mechi za awali dhidi ya Rwanda, Ethiopia na Burundi ambapo Tanzania ilitawala na kufunga mabao kwa urahisi, safu ya ulinzi ya Sudan ilikuwa imara na kuzuia mianya yote ya ushambuliaji. Kwa upande mwingine, safu ya ulinzi ya Tanzania nayo ilikaa imara kudhibiti kasi ya Sudan iliyotoka kuifunga Uganda mabao 3-2.

Mchezo huo uliendelea kuwa wa mbinu za hali ya juu na kusubiri makosa hadi dakika 90 za kawaida zilipomalizika kwa suluhu ya 0-0 kabla ya kuingia muda wa ziada.

Uganda Yakung’uta Burundi na Kutwaa Medali ya Shaba

Katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, timu ya Taifa ya Uganda U20 ilifanikiwa kuondoka na medali ya shaba baada ya kuichapa Burundi mabao 2-0.

Derrick Ssozi aliifungia Uganda bao la kwanza katika dakika ya 22 kufuatia pasi safi ya Elvis Opakrwoth. Burundi walijaribu kurudi mchezoni lakini kipa wa Uganda, Adrian Isabirye, na safu yake ya ulinzi walisimama imara. Kyakuwa alihitimisha ushindi wa Uganda kwa kufunga bao la pili dakika za mwisho za mchezo akipokea pasi kutoka kwa Steven Oyirwoth.

Kutoka Biharamulo Mpaka Jason Derulo: Historia na Mafanikio ya Dansa Rany Kida