Wababe wa Dunia Kushuka Dimbani Leo
Kivumbi kuwaka kwenye mechi mbalimbali leo za Mataifa ambapo kila timu inahitaji ushindi mkubwa leo. Je nani na nani kuondoka na pointi 3 za uhakika?
Kundi A, kutakuwa na mechi ya kukata na shoka kati ya Ufaransa dhidi ya Italia moja ya mechi kubwa katika hatua ya makundi ya UEFA Nations League. Ufaransa imeanza vyema chini ya kocha mpya Zinedine Zidane, ikiwa imeshinda mechi zake mbili za kwanza dhidi ya Uturuki na Ubelgiji kwa matokeo ya 1-0. Italia nayo imeonyesha dalili za kuimarika, hasa baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Uturuki.
Bado Ufaransa iaendelea kumkosa nahodha wake Kylian Mbappé, ambaye alipata jeraha baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Uturuki. Hata hivyo, kikosi cha Zidane kina kina kikubwa cha vipaji, huku Ousmane Dembélé, Michael Olise, Bradley Barcola na Désiré Doué wakiwa na uwezo wa kuleta tofauti katika eneo la mwisho.
Italia, chini ya Roberto Mancini, inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na matumaini baada ya kuifunga Uturuki 4-1. Mancini amefanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi, akiwapa nafasi wachezaji wapya kadhaa kama sehemu ya kujenga timu mpya baada ya kipindi kigumu cha kutofuzu Kombe la Dunia.
Mechi hii unaweza kuipata kule Meridianbet ambapo pia unaweza ukapata kujua misimamo ya makundi yote ya michuano hii ya UEFA Nations League.
Italia inaweza kujaribu kutumia nguvu na nidhamu ya Sandro Tonali, Davide Frattesi na Niccolò Fagioli, huku Ufaransa ikiwa na uwezo wa kuvunja mistari kupitia kasi na ubunifu wa viungo na mawinga wake.
Kwa ujumla, Ufaransa inaonekana kuwa na faida kutokana na kucheza nyumbani, kina cha kikosi na mwanzo mzuri wa Zidane, lakini Italia imeonyesha kwamba inaweza kufunga mabao mengi ikiwa itaachiwa nafasi. Hivyo, siioni kama mechi rahisi kwa Ufaransa.
Nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi wanapewa Ufaransa kutokana na kiwango chao ambacho wanacho. Je nani unampa nafasi ya kushinda?.
Kivumbi kitawaka kwenye mechi ya Ubelgiji dhidi ya Uturuki kwenye michuano ya UEFA Nations League huku tofauti yao hadi sasa ni pointi 3 mpaka sasa kwani Uturuki mpaka sasa hawajashinda mechi yoyote kwenye mbili walizocheza.
Ubelgiji wamekusanya pointi 3 baada ya kuifunga Italia huku leo hii pia wanahitaji ushindi ili kuweza kukaa kwenye nafasi nzuri. Uturuki, kwa upande mwingine, imepoteza mechi zote mbili 1-0 dhidi ya Ufaransa na 4-1 dhidi ya Italia hivyo presha ipo zaidi kwa upande wao.
Kama inavyojulikana kila timu huwa ina mchezaji au wachezaji muhimu zaidi ambao huamua matokeo na kwa upande wa Ubelgiji, Kevin De Bruyne bado ni mhimili, huku nguvu yao ikiwa kwenye uwezo wa kutawala mpira na kutengeneza nafasi kupitia safu ya kiungo na pembeni.
Timu hiyo pia inaonekana kuwa na ubora zaidi katika kumalizia nafasi, jambo ambalo linaweza kuwa tatizo kwa Uturuki ambayo imefunga bao moja pekee katika mechi mbili za kwanza za Nations League.
Licha ya kupoteza mechi zote mbili, Uturuki sio timu ya kudharauliwa na Arda Güler ndiye mchezaji anayetarajiwa kuleta ubunifu na kasi katika mashambulizi. Tatizo kubwa kwa Uturuki ni kwamba safu yao ya ulinzi ilionekana dhaifu sana dhidi ya Italia, na dhidi ya Ubelgiji kosa kama hilo linaweza kuigharimu zaidi.
Mara ya mwisho kuonana ilikuwa ni 2011 na hakuna ambaye alikuwa mbabe kati yao. Je leo hii nani kuondoka na ushindi?.