Dabi ya Kariakoo Simba na Yanga
Yanga SC

Dabi ya Kariakoo Leo: Simba na Yanga Kukipiga Uwanja wa Uhuru!

Vardo October 10, 2026 8:15 am

Zilizokuwa miezi, wiki na siku, sasa ni saa chache tu zinazohesabika kuelekea pambano kubwa la Dabi ya Kariakoo kati ya miamba ya soka nchini, Simba na Yanga, litakalopigwa leo saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kisu na nyembe kutokana na historia ndefu na ushindani wa jadi kati ya timu hizi mbili. Kadri muda unavyosogea, presha ya mashabiki inazidi kupanda, kila upande ukisubiri kwa hamu kuona timu yake ikiibuka kidedea. Simba ndio wenyeji wa mchezo huu wa leo, ambapo mbali na pointi tatu, ni suala la heshima na fahari kubwa kwa mashabiki wao.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi, amefichua kuwa kikosi chake kimefanya utafiti wa kina na kinatambua maeneo yote ya hatari kutoka kwa wapinzani wao Simba. Amesisitiza kuwa maandalizi yao yamelenga kuzima ubora wa Simba, hasa namna wanavyotumia udhaifu wa wapinzani wao kupata mabao.

“Mipira iliyokufa ni miongoni mwa silaha hatari za Simba, kwani wana wachezaji wenye uwezo mzuri wa kutumia mipira ya adhabu na kona,” alisema Mngqithi.

Kocha huyo alieleza kuwa Yanga imejipanga kuhakikisha Simba haipati nafasi ya kufika kwenye maeneo hatari karibu na lango lao ili kuzuia faulo na kona zinazoweza kuzaa mabao ya ghafla.

Katika mchezo huu wenye ushindani mkubwa, nidhamu ya wachezaji na utekelezaji wa maelekezo ya makocha ndio utakaotoa uamuzi. Je, ni Simba itakayotumia vizuri uwanja wa nyumbani au Yanga itatekeleza mpango wake wa ushindi?

Ujumbe Mzito wa Neo Maema kwa Wachezaji wa Simba SC Kuelekea Kariakoo Dabi