Kocha wa Simba Steve Barker
Simba SC

Kocha wa Simba Steve Barker: Hakuna Muda wa Kusherehekea Dabi!

Vardo October 11, 2026 3:42 pm

KOCHA wa Simba, Steve Barker, ameweka wazi kuwa hakuna nafasi ya kujivunia au kusherehekea kwa muda mrefu ushindi wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga. Badala yake, amesisitiza kuwa kikosi chake kinapaswa kuelekeza nguvu zote katika maandalizi ya michezo inayofuata ili kulinda moto wao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hivi karibuni, Simba iliibuka na ushindi mtamu wa mabao 2-1 dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga, kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Ushindi huo sio tu umeongeza morali kikosini, bali pia umeifanya Simba kufikisha ushindi wa mechi saba mfululizo msimu huu.

Licha ya kufanya vizuri dhidi ya vigogo kama Yanga na Azam FC, Kocha Steve Barker amewataka wachezaji wake kupunguza shangwe na kurejea haraka kwenye mstari.

“Ni muhimu kufurahia ushindi jana lakini leo tunapaswa kuanza upya kwa sababu tuna mchezo muhimu dhidi ya Mashujaa katikati ya wiki, pamoja na majukumu ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” amesema Barker.

Simba haina anasa ya kupumzika kwani inakabiliwa na ratiba ngumu inayowataka wachezaji kuonyesha nidhamu ya juu, umakini, na mwendelezo wa kiwango bora (consistency) katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Kwa upande wa klabu na mashabiki, ushindi wa Dabi ya Kariakoo ni chachu kubwa ya kujiamini, lakini kama anavyokumbusha Barker, thamani halisi ya ushindi huo itaonekana endapo timu itaendeleza wimbi hilo la ushindi kwenye mechi zinazofuata.

Siri ya Ushindi wa Simba 2-1 Dhidi ya Yanga Dabi ya Kariakoo Kwanini Mabadiliko ya Mngqithi Yanga Yaliwagharimu Dhidi ya Simba?