Manqoba Mngqithi
Yanga SC

Manqoba Mngqithi Amekiri Simba Dabi, Afichua Siri ya Yanga Kupoteza

Vardo October 12, 2026 11:40 am

Kocha Mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi, amevunja ukimya na kukiri ubora wa Simba katika mchezo mkali wa Dabi ya Kariakoo uliomalizika kwa Yanga kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Wekundu wa Msimbazi. Mngqithi amefichua namna wapinzani wao walivyoongeza presha na kutumia udhaifu wa kikosi chake kuamua matokeo.

Akizungumzia mwenendo wa mchezo huo, Mngqithi amesema Yanga ilianza vizuri na kuonyesha ushindani wa hali ya juu, huku ikifanikiwa kufunga bao zuri na kutengeneza nafasi kadhaa kabla ya mapumziko. Hata hivyo, ukosefu wa umakini katika eneo la mwisho la ushambuliaji uliigharimu timu hiyo.

“Tulionyesha sehemu ya uwezo wetu na kufunga bao zuri. Pia, tulitengeneza nafasi chache kabla ya mapumziko, lakini hatukuwa makini vya kutosha katika eneo la mwisho la ushambuliaji,” alisema Mngqithi.

Kupoteza Uwiano na Kujilinda

Kocha huyo aliongeza kuwa, pamoja na kuanza kwa kasi nzuri na kumiliki mpira, Yanga ilianza kupoteza uimara na nguvu katika safu ya ulinzi kadri muda ulivyokuwa unasonga. Hali hiyo iliwapa Simba mwanya wa kuongeza makali ya mashambulizi na kubadilisha mwelekeo wa mchezo huo wa Ligi.

“Pamoja na kwamba tulikuwa tunacheza vizuri tulipokuwa na mpira, katika upande wa kujilinda tulipoteza nguvu tulizokuwa nazo mwanzoni mwa mchezo,” alieleza.

Simba Walitumia Makosa Yetu

Mngqithi alikiri kuwa Simba ilitumia kikamilifu vipindi ambavyo Yanga ilipoteza uwiano uwanjani, ikishambulia kwa kasi na kuwalazimisha wachezaji wake kufanya makosa yaliyowagharimu mabao.

“Simba walitusukuma sana na kutulazimisha kufanya makosa. Walikimbia sana katika kipindi cha pili, nasi tulijaribu kufanya marekebisho ili kuboresha mchezo wetu, lakini kwa bahati mbaya tulichelewa. Juhudi zetu hazikutosha siku hiyo na lazima tuwape Simba heshima kwa ushindi wao,” alihitimisha.

Mohamed Shillaarejea AIK Sweden Baada ya Majukumu ya Taifa U-23 Alichosema Ali Kamwe Baada ya Yanga Kupoteza Dabi ya Kariakoo