Djigui Diarra
Yanga SC

Yanga SC Yamkinga Djigui Diarra, Yataja Mbadala Wake Halisi!

Vardo October 20, 2026 7:30 am

Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe, amewatoa hofu mashabiki na wanachama wa klabu hiyo akisema kuwa kikosi hakina presha yoyote kuhusu ukosefu wa mlinda mlango wake namba moja, Djigui Diarra, ambaye anaendelea kupumzika na kupata matibabu.

Kamwe amesisitiza kuwa makipa Aboutrika Bonsheri na Hussein Masalanga wana uwezo mkubwa wa kulinda ngome ya timu hiyo bila shida yoyote.

“Wanayanga wote wamejionea kiwango cha Aboutrika Bonsheri. Ameonyesha ubora mkubwa, kiasi kwamba hata Djigui Diarra akiendelea kupumzika na kupata matibabu, hakuna sababu ya kuwa na presha kwa sababu bado tunaye Hussein Masalanga, kipa mwenye uzoefu wa kutosha,” alisema Kamwe.

Hali ya Wachezaji Majeruhi na Waliorejea

Wakati huohuo, Kamwe amewataja wachezaji watakaokosekana katika mchezo ujao wa Jumatano kutokana na majeraha kuwa ni pamoja na Yao Attola (anayesumbuliwa na misuli ya nyuma ya paja), Casemiro, na Saleh Osi, ambao wanaendelea na matibabu.

Hata hivyo, Yanga imepata nguvu mpya baada ya kurejea kwa beki kisiki Dickson Job (BBD – Big Brain Defender), ambaye amepokea ruhusa ya kushiriki michezo ya ushindani baada ya kupona jeraha lake. Vilevile, mshambuliaji hatari Clement Mzize yuko tayari kabisa kuendelea na majukumu ya kuipambania timu hiyo.

Licha ya changamoto za majeraha, Yanga ipo katika hali nzuri ya kiushindani na inaendelea na maandalizi ya mwisho kuhakikisha inavuna ushindi kwenye mchezo ujao.

Anathiel Chilambo: Kikosi cha Simba Kipo Tayari Kazi CAF! Yanga Yamtisha CFFA! MVUA YA MBAO Inakuja Jumatano