Sead Ramovic kurejea Yanga SC
Yanga SC

Sead Ramovic Kurejea Yanga SC: Kutua Kesho Mchana Kukamilisha Mkataba Mapya!

Vardo October 30, 2026 8:11 am

Kocha mpya wa Yanga SC, Sead Ramovic, anatarajiwa kuwasili nchini kesho mchana kwa ajili ya kukamilisha taratibu zote za kujiunga na miamba hiyo ya Msimbazi na Jangwani. Ramovic anakuja kusaini mkataba rasmi na kuanza majukumu yake mapya ya kukinoa kikosi hicho.

Kuwasili kwa Ramovic kunamfanya aanze safari yake ya pili ndani ya Yanga SC. Hatua hii inajiri baada ya uongozi wa klabu kumwamini tena na kumpa benchi la ufundi kufuatia kuondoka kwa kocha Manqoba Mngqithi, aliyefungashiwa virago kutokana na mfululizo wa matokeo yasiyoidhisha.

Mngqithi aliondoka klabuni hapo baada ya Yanga kupoteza mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba SC, matokeo yaliyofuatiwa na sare ya bao 1-1 dhidi ya TRA United — matokeo yaliyoingiza presha kubwa kwa benchi la ufundi na uongozi.

Kushuhudia Mchezo Dhidi ya Kagera Sugar

Baada ya kukamilisha taratibu za mkataba, Ramovic anatarajiwa kuungana na mashabiki wa Wanayanga na wadau wa soka kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara siku ya Jumapili. Yanga SC itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge.

Mchezo huo utakuwa fursa nzuri kwa kocha huyo mpya kuanza kukisoma kikosi chake kwa ukaribu na kupata picha halisi ya hali ya timu kabla ya kushika rasmi mikoba ya ufundi mazoezini.

Kurejea kwa Ramovic kunafungua ukurasa mpya wa matumaini ndani ya Yanga SC, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona mbinu zake zikirejesha makali ya timu, kuboresha matokeo, na kuendeleza ushindani kwenye mechi zinazofuata.

Rushine De Reuck Aibuka Shujaa Simba SC: “Pointi 3 Ndicho Kiitu cha Muhimu” Steve Barker: Sio Kila Siku Tutacheza Vizuri, Muhimu ni Pointi Tatu!