ORODHA YA NYOTA SABA WA SIMBA WATAKAOIKOSA DABI LEO KWA MKAPA
LEO Kikosi cha Simba kitakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu muhimu mbele ya watani zao wa jadi Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara huku kikikosa huduma ya nyota wake 7 wa kikosi cha kwanza.Unakuwa ni mchezo wa kwanza kukutana kwenye dabi kwa mzunguko wa kwanza ambapo Yanga ni wenyeji na wapo nafasi ya pili baada ya kucheza...
MPINZANI WA MWAKINYO ATIA TIMU BONGO KUTOKA ARGENTINA NA TAMBO KIBAO
JOSE Carlos Paz, atakayezichapa na Hassan Mwakinyo Novemba 13 kwenye ukumbi wa Next Door Arena Oysterbay amewasili na kutamba kutwaa ubingwa wa uzito wa Super Welter wa WBF unaoshikiriwa na Hassan Mwakinyo.Bondia huyo raia wa Argentina amewasili na baba yake Alberto Ramon Paz ambaye pia ni kocha wake kama ilivyo kwa bondia Floyd Mayweather.Akizungumza mara baada ya kuwasili, Paz amesema kuwa...
SERIKALI YAWAPA ONYO WANG’OA VITI KWENYE DABI YA KESHO
KUELEKEA mchezo wa watani wa jadi, Yanga dhidi ya Simba, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, ametoa onyo kali kwa wale watakaothubutu kung’oa viti na kufanya vurugu kwenye mchezo huo.Msimu wa 2016/17, timu hizo zilicheza ambapo zilitoka sare ya bao 1-1, bao la Yanga lilifungwa na Amisi Tambwe ambapo mashabiki wa Simba...
U 17 YABANWA MBAVU LEO AFRIKA KUSINI
BAADA ya mchezo wa kwanza wa wa ufunguzi kwenye mashindano ya Cosafa yanayofanyika nchini Afrika Kusini leo timu ya Taifa ya Wanawake ya U 17 imepoteza kwa kufungwa mabao 2-1.Mchezo wa kwanza kwa U 17 iliyo chini ya Kocha Mkuu, Edna Lema ambaye ameweka wazi kuwa wachezaji wapo vizuri katika kupambana ili kupata matokeo chanya ilishinda kwa mabao 5-1.Ilikuwa...
MTIBWA SUGAR: MSIMU HUU USHINDANI NI MKUBWA
THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 ni mkubwa jambo ambalo linalowapa matokeo ya tofauti ndani ya uwanja.Kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Novemba Mosi dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba Mtibwa Sugar iliyeyusha pointi tatu mazima kwa kufungwa mabao 2-1 .Licha ya kuweka rekodi ya kuwa...
CHAMA KUIKOSA YANGA UWANJA WA MKAPA KESHO
MAMBO ni mazito kwa mabingwa watetezi Simba ambao kesho wanakutana na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa na huenda kesho wakakosa jumla huduma ya mtambo wao wa mabao Clatous Chama.Simba ikiwa imefunga mabao 21 Chama amehusika kwenye mabao saba ambapo ametoa pasi tano za mabao na kutupia mabao mawili.Kwenye mechi mbili ambazo hakuwepo kikosi cha...
KOCHA SIMBA HANA CHAGUO LA KWANZA
KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, amewachambua washambuliaji wake wote, huku akidai kuwa bado hana chaguo la kwanza na kudai kwamba atawatumia kulingana na michezo husika. Simba kwa sasa ina washambuliaji wa kati wanne ambao ni Meddie Kagere, John Bocco, Chris Mugalu na Charles Ilanfya ambao kwa pamoja wameifungia timu hiyo mabao 10 katika michezo ya Ligi Kuu Bara...
KOCHA YANGA AWAPIGA MKWARA SIMBA, KUMALIZA KAZI DAKIKA 20 KESHO
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze, amewaambia vijana wake kuwa, katika mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Simba, anataka bao ndani ya dakika 20 kipindi cha kwanza kwa lengo la kuwaondoa mchezoni wapinzani wao hao. Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara. Katika kuelekea mchezo huo, Jumatano usiku kikosi...
MTAMBO WA MABAO SIMBA HATMA YAKE KUIVAA YANGA KESHO MIKONONI MWA SVEN
MSHAMBULIAJI wa Simba, Mkongomani, Chris Mugalu, amerejesha matumaini kwenye kikosi cha timu hiyo katika kuelekea Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga, Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar. Mkongomani huyo alikuwa nje ya uwanja kwa michezo mitatu akiuguza maumivu ya nyonga ambayo ni dhidi ya Tanzania Prisons, Ruvu Shooting na Mwadui FC.Daktari mkuu wa timu hiyo, Yassin Gembe, amesema mshambuliaji...
ORODHA YA WAAMUZI NANE WA YANGA V SIMBA KESHO HII HAPA
KESHO Novemba 7 Uwanja wa Mkapa kutakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Simba majira ya saa 11:00 jioni. Hii hapa orodha ya waamuzi wa mchezo huo ambao umeshika hisia za wadau