CORONA YATIBUA MAMBO MBEYA CITY
UONGOZI wa Mbeya City umesema kuwa unaendelea kuomba dua usiku na mchana hali ikae shwari ili maisha yaendelee kama zamani.Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mbeya City, Shaha Mjanja amesema kuwa wanashindwa kuendelea na program za kawaida kutokana na kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona."Kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona tumeshindwa kuendelea na program ambazo zilikuwa zimepangwa...
MFUMANIA NYAVU WA YANGA AWAPA NENO HILI MABOSI WAKE
AMIS Tambwe, mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Simba amesema kuwa Yanga inahitaji kufanya usajili makini ambao utawapa matokeo chanya msimu ujao.Akizungumza na Saleh Jembe, Tambwe ambaye msimu uliopiota akiwa ndani ya Yanga alifunga mabao 12 amesema kuwa anaamini viongozi wanatambua aina ya wachezaji ambao wanawahitaji."Nimekuwa Yanga na ninatambua kwamba kuna viongozi ambao wanajua wajibu wao hivyo ni muhimu...
USAJILI WA PACHA ZA NAMUNGO NDANI YA YANGA UMESHIKILIWA NA HUYU HAPA
IMEBAINIKA kuwa kwa sasa mabosi wa Yanga wanasubiria kauli ya kocha wao Luc Eymael tu kwa ajili ya kumalizana na mastaa wawili Lucas Kikoti na Reliants Lusajo ambao wanawawinda kwa wakati huu.Kikoti na Lusajo wamekuwa na msimu bora wakiwa na kikosi chao cha Namungo FC cha Lindi ambapo wamehusika kwenye mabao 14, huku Lusajo akifunga 11 na Kikoti manne.Habari...
CHEKI PICHA PICHA SOSO AKIUAGA UKAPERA
HIZI hapa picha za beki wa Yanga Ally Mtoni akiuaga ukapera
BEKI SIMBA SASA AGEUKIA MAPISHI
PASCAL Wawa raia wa Ivory Coast amesema kuwa kwa sasa amekuwa akitumia muda mwingi katika upishi kwa kujipikia vyakula anavyopenda kila baada ya kumaliza mazoezi kutokana na kuwepo kwa Ugonjwa wa Covid-19 unaosambazwa na Virusi vya Corona.Wawa ametoa kauli hiyo kutokana na kitendo chake cha kuonyesha video zake katika mitandao ya kijamii akiwa anapika vyakula vyenye asili ya kwao...
NONGA ANAWAPA TABU KWELI LIPULI FC KWA SASA
PAUL Nonga, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Lipuli FC chenye maskani yake mkoani Iringa anawapa tabu mabosi wake hao kwa sasa kumtafuta mbadala wake.Nonga ameliambia Championi Ijumaa kuwa tayari amewajulisha viongozi wake kuanza kutafuta mbadala wake pale mkataba wake utakapomalizika Juni Mosi, 2020 kwa kuwa anahitaji changamoto mpya.Championi Ijumaa lilimtafuta Ofisa Habari wa Lipuli FC, Clement Sanga...
MPISHI WA MABAO YANGA AKUMBUKA UFUNDI WA MORRISON, AOMBA LIGI IREJEE
JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga, amesema kuwa anaomba dua usiku na mchana janga la Virusi vya Corona lipite ili ligi irejee kutokana na kukumbuka madude ya kiungo wao, Bernard Morrison.Abdul amesema kuwa kwa sasa wamekuwa wanyonge nyumbani kutokana na kushindwa kuendelea kucheza baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa na Serikali.“Kuna mambo mengi ambayo nimekumbuka ndani ya ligi ikiwa...
SIMBA SC YAKOMBA MABEKI WOTE STARS
SIMBA ipo katika mawindo ya kuimarisha kikosi chake kwa msimu ujao wa ligi na michuano ya kimataifa, endapo itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Katika mawindo hayo, Simba inatarajia kufanya kufuru kubwa kwa kung’oa vifaa vyote hatari ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.Baada ya kudaiwa kumalizana na beki wa kati, Bakari Mwamnyeto ‘Nondo’, anayechezea...
BORUSSIA DORTMUND WAIGANDA SAINI YA SANCHO
BORUSSIA Dortmund imeripotiwa kuwa imeanza mazungumzo na mchezaji wao Jadon Sancho ili aongeze mkataba wake kuendelea kubaki Klabuni hapo.Nyota huyo mwenye miaka 20 amekuwa akipigiwa hesabu na timu nyingi ambazo zinashiriki Ligi Kuu England.Manchester United na Chelsea ni miongoni mwa timu zinazotajwa kuiwinda saini ya nyota huyo.Mkataba wake wa sasa unameguka mwaka 2022 hivyo mabosi wa Dortmund wanataka wamuongeze...
CHAMA ATIBUA DILI LA MKUDE, NDEMLA YANGA
WACHEZAJI wawili ndani ya kikosi cha mabingwa watetezi Ligi Kuu Bara Simba ambao wote ni viungo, Jonas Mkude na Said Ndemla, watakuwa wamepoteza dili lao Yanga kufuatia sakata la hivi karibuni lililomuhusisha Mzambia Clatous Chama ikidaiwa kufanya mazungumzo na kiongozi wa Wanajangwani.Hivi karibuni ilitokea msuguano kati ya uongozi wa timu hizo mbili, baada ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick...