KOCHA YANGA : WACHEZAJI WALIKUWA WAMEINGIA KWENYE MFUMO
LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hesabu zake ni kuona timu yake inamaliza ikiwa nafasi ya pili jambo ambalo anaamini linaweza kufanikiwa kwa kuwa wachezaji walikuwa wameanza kuingia kwenye mfumo.Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kwa muda kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona.Eymael amekiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi 15 ambazo ni sawa na dakika...
KOCHA MKUU WA SIMBA ATAJA KITAKACHOMREJESHA MLIPILI KIKOSI CHA KWANZA
SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa beki wa Simba Yusuph Mlipili anatakiwa kuongeza juhudi ili kupata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza.Mlipili ndani ya Simba msimu huu hajawa na nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kutokana na kile kinachoelezwa ni ushindani wa namba ndani ya kikosi cha Simba.Kwa sasa Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 71...
MUONEKANO WA UKURASA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI
MUONEKANO wa Ukurasa wa mbele Gazeti la CHAMPIONI Jumamosi, nafasi ya kushinda ndinga ni yako
MENEJA WA MAKAMBO AMRUHUSU KUTUA YANGA
KOCHA wa zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema kuwa kama kweli klabu hiyo inataka kumrejesha mshambuliaji wao wa zamani, Heritier Makambo, anayekipiga Horoya ya Guinea kwa sasa, wafanye hivyo haraka ila wawe na uhakika wa kumlipa mshahara mzuri.Zahera ambaye inaaminika kuwa ndiye Meneja wa mchezaji huyo, amesema kwake yeye haoni tatizo la Makambo kurudi Yanga baada ya klabu hiyo...
GALLAS: NINAWEZA KUCHEZA NDANI NA NJE YA BONGO
WILLIAM Lucian, ‘Gallas’ beki wa kuliwa wa Polisi Tanzania amesema kuwa ana uwezo wa kucheza popote ndani ya Bongo na nje pia.Polisi Tanzania ipo nafasi ya sita ikiwa imecheza mechi 29 ina pointi 45 imefunga mabao 29 na safu ya ulinzi imeruhusu mabao 26, kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.Akizungumza na Saleh...
BARCELONA WAINGIA ANGA ZA KUIWNDA SAINI YA NYOTA WA UNITED GOMES
GOMES Angel nyota anayekipiga ndani ya Manchester United amewekwa kwenye rada na Barcelona.Kinda huyo anayekipiga ndani ya United mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.Gomes ana miaka 19 anataka kutimka ndani ya kikosi hicho licha ya United kumpa ofa ya pauni 25,000 kwa wiki.Uwezo wake umewavutia vigogo ndani ya La Liga hivyo kuna uwezekano United wakaikosa huduma yake.
YANGA SASA KUFUATA JEMBE JINGINE LA KAZI AS VITA
INAELEZWA kuwa Yanga imeingia kwenye anga za kuiwinda saini ya Rossein Tuisila Kisinda. Winga huyo mwenye umri wa miaka 20 anakipiga ndani ya Klabu ya AS Vita inayoshiriki Ligi Kuu ya DR Congo akiwa na uwezo wa kufunga pia.Watani zao wa jadi Simba waliingia kwenye anga za kuiwinda saini ya nyota huyo mipango yao iligonga mwamba.
UBINGWA WA LIVERPOOL MASHAKANI IWAPO MSIMU WA 2019/20 UTAFUTWA
IWAPO msimu wa 2019/20 wa Ligi Kuu England ukifutwa, Liverpool inabidi isahau kutwaa ubingwa licha ya kwamba inaongoza ikiwa na pointi 82 kibindoni.Mamlaka za soka barani Ulaya wameeleza kuwa Kuna uwezekano mkubwa wa msimu huu wa 2019/20 kufutwa ikiwa shughuli za soka hazitarejea hadi kufikia Juni mwaka huu.Aleksandr Ceferin, Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) amesema kuwa kuna...
ALICHOKISEMA AUSSEMS KUHUS JONAS MKUDE
ALIYEKUWA Kocha wa Simba SC, Patrick Aussems amemtaja Jonas Mkude kuwa ni miongoni mwa wachezaji muhimu ambao waliifanya timu hiyo kufanya vizuri katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018/19.Simba ikiwa chini ya kocha huyo raia wa Ubelgiji alifika hadi hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo waliondolewa kwa kufungwa jumla ya mabao 4-1...