Uncategorized

SIMBA: HAIKUWA RAHISI KUFIKA HAPA

admin May 28, 2019 10:34 pm


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kwao kutwaa ubingwa kwani walicheza mfululizo hasa kipindi cha mwisho ila juhud zimewapa walichokuwa wanastahili.

Aussems amesema kuwa wachezaji wake walikuwa wamechoka kutokana na kucheza michezo 15 ndani ya siku 30 ila hawakuwa na jinsi zaidi ya kutafuta matokeo.

“Haikuwa safari nyepesi kufika hapa, tumecheza michezo mingi ile ya karibu ikiwa ni 15 ndani ya siku 30 ni ngumu sana kupata matokeo chanya muda wote.

“Kwa upande wa waamuzi muda wote nimekuwa nikiona wakifanya majukumu yao ila sikupaswa kujali kwa kuwa wanatimiza majukumu yao ingawa kuna wakati walikuwa wanafanya maamuzi ambayo yanatuumiza sisi pamoja na wapinzani wetu,” amesema.

MUONEKANO WA GAZETI LA CHAMPIONI KATIKA UKURASA WA MBELE LEO JUMATANO YANGA YATAJA KILICHOIPONZA KUKOSA UBINGWA MSIMU HUU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply