Home Uncategorized HAWA HAPA WALIOTWAA TUZO ZA MO

HAWA HAPA WALIOTWAA TUZO ZA MO

USIKU wa tuzo za MO zilizofanyika katika Ukumbi wa Hyatt Regency, ambapo muwekezaji wa Klabu ya Simba, Mo Dewji, ametoa tuzo kwa wachezaji wa klabu hiyo katika vipengele tofauti tofauti, hii hapa orodha ya washindi wa tuzo hizo:-

Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka ya Mo Simba 2019 ni Meddie Kagere.

Goli la Clatous Chama dhidi ya Nkana limeshinda Tuzo ya Goli Bora la Mwaka.

Tuzo ya Heshima inakwenda kwa Azim Dewji.

Meddie Kagere ameshinda Tuzo ya Mfungaji Bora wa Mwaka.

Erasto Nyoni ameshinda Tuzo ya Wachezaji.

Mwanahamisi Omary Shurua ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Mwanamke wa Mwaka.

Rashid Juma ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka.

John Bocco ameshinda Tuzo ya Mshambuliaji Bora wa Mwaka.

James Kotei ameshinda Tuzo ya Kiungo Bora wa Mwaka.

Erasto Nyoni ameshinda Tuzo ya Beki Bora wa Mwaka.

Aishi Manula ameshinda Tuzo ya Golikipa Bora wa Mwaka.
SOMA NA HII  DODOMA FC YASAJILI WAPYA WATATU