Home Uncategorized TANZIA: MJUMBE KAMATI YA UTENDAJI YANGA AFARIKI

TANZIA: MJUMBE KAMATI YA UTENDAJI YANGA AFARIKI


TIMU ya Yanga pamoja na familia ya wanamichezo duniani imepata pigo kufuatia kifo cha mjumbe wa kamati ya Yanga Felix Kibodya.

Kibodya amefariki usiku wa kuamkia leo Ijumaa hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amethibitisha taarifa hizo za kifo cha Kibodya.
Mwakalebela amesema Yanga imepata pigo kutokana na msiba huo kwani walikuwa wanategemea nguvu kubwa kutoka kwa marehemu juu ya taaluma yake ya sheria.

Mwakalebela ameongeza kuwa kwa sasa klabu yao inafuatilia msiba huo kwa karibu kujua utaratibu kamili na kwamba baada ya hapo watatoa taarifa.

SOMA NA HII  VIFUAVIWILI:WATANIELEWA TU SIKU MOJA LICHA YA KUNIBEZA KWA SASA