Home Uncategorized Meddie Kagere akabidhiwa tunzo yake.

Meddie Kagere akabidhiwa tunzo yake.

Moja ya dhumuni kuu la tovuti yetu ni kusheherekea mafanikio ya watu ambao wanafanya vizuri katika ulimwengu huu wa soka kwa Tanzania. Toka mwanzo wa msimu wa Ligi Kuu Tanzania bara, tovuti imekuwa ikitoa zawadi kwa wafungaji bora kila mwezi, ikiwa na lengo la kutambua mchango wao.

Msimu wa ligi kuu 2018/2019 umemalizika na Meddie Kagere ameibuka kuwa galacha wa mabao wa ligi kuu, akifunga mabao 23 akiwa na klabu yake ya Simba SC na kuisaidia kuchukua ubingwa kwa mara nyingine.

Tovuti yetu imemkabidhi zawadi yake ya Galacha wa Magoli msimu wa 2018/2019, ikiwa ni sehemu ya kutambua kile alichofanya.

“Ninashukuru sana kwa tunzo hii, hakika ni kitu kikubwa sana kwangu kutoka kandanda.co.tz” alituambia kwa furaha mara baada ya kupokea tunzo hii.

Huu utaendelea kuwa utaratibu wa tovuti yetu kwa msimu ujao pia, ikiwa pamoja na kuwatunuku zawadi wachezaji wanaoongoza kwa ufungaji wa mabao kila mwezi.

 

The post Meddie Kagere akabidhiwa tunzo yake. appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  MAALIM BUSUNGU: LIKIJA DILI KUBWA NASAINI