SAMATTA: SIKUTARAJIA KUPEWA TUZO MBILI, KAZI INAANZA LEO NIFUATE
Mbwana Samatta nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania,’Taifa Stars’ amesema kuwa hakutarajia kupewa tuzo za heshima na uongozi wa Global Group jambo ambalo limemshangaza alipotembelea ofisi za Global Group jana.
Samatta ambaye anayekipiga KRC Genk, leo atakuwa uwanja wa Taifa kumenyana na timu Kiba, kwenye mchezo wa hisani wenye lengo la kurudhisha thamani kwa jamii inayowazunguka hasa yenye mahitaji.
Akizungumza na Saleh Jembe baada ya kupewa tuzo mbili kutokana na mafanikio makubwa aliyopata katika msimu uliopita baada ya kuipa ubingwa timu yake pamoja na kufunga mabao 23 akiwa nyuma ya mfungaji bora amesema kuwa :- “Sikutarajia kupewa tuzo hizi, ni jambo kubwa na linalonipa hasira ya kupambana nasema asante kwa sapoti yenu na zawadi ambazo mmenipa ni jambo la faraja kwangu,”.
“Nitafanya kwa vitendo siku zote na kwa kuanza mashabiki wangu wasikose kujitokeza uwanja wa Taifa kuona namna nitakavyoifanya timu Kiba, kwenye Nifuate Project,” amesema.

Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.