Home Uncategorized LACAZETTE AIBUA MASWALI KUPITA MITAA YA BARCELONA

LACAZETTE AIBUA MASWALI KUPITA MITAA YA BARCELONA


STRAIKA wa Arsenal, Alexandre Lacazette ameonekana katika mitaa ya jiji la Barcelona juzi na kuzua maneno.

 Baada ya kuonekana huko, ndio wadau wa soka wakadai kuwa Lacazette huenda ametua kukutana na viongozi wa klabu ya soka.
Barcelona inajulikana inasaka straika wa kati na miongoni mwa mastaa akiwemo Lacazette . Lacazette amepachika mabao 19 katika mechi 48 ambazo ameichezea Arsenal msimu wa 2018/19.
Klabu hiyo inatafuta mbadala wa Luiz Suarez, ambaye umri unazidi kumtupa mkono akiwa na umri wa miaka 32. Ili kumpata straika huyo basi Barcelona itapaswa kupanga bajeti ya kiasi cha pauni milioni 57.
Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa fowadi huyo yupo kwa mapumziko katika mji wa Barcelona baada ya kumalizika kwa msimu.
SOMA NA HII  YANGA KUISHUSHA SIMBA KILELENI