Home Uncategorized RAMADHAN KABWILI BADO HAKIJAELEWEKA YANGA, APATA DILI NJE

RAMADHAN KABWILI BADO HAKIJAELEWEKA YANGA, APATA DILI NJE

MLINDA mlango wa Yanga Ramadhani Kabwili amesema bado hawajafikia muafaka na mabosi wa timu moja nchini Sudan.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kabwili alisema; “Mkataba wangu na Yanga umekwisha na bado sijaongeza mkataba mwingine, kwa sasa naendelea na mipango yangu mingine ikiwa ni pamoja na kuangalia ofa ambazo nipo nazo mkononi.”
“Kuna timu moja ipo nchini Sudan ambayo inahitaji huduma yangu wakati ukifika nitaweka wazi kila kitu.

“Kipaumbele changu cha kwanza ni timu yangu ya Yanga ofa yao lazima niifanyie kazi ukizingatia wao ndiyo wamenilea na kunifikisha hapa nilipo, ni suala la wakati,” alisema Kabwili.
SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA SC KINACHOANZA DHIDI YA ASEC MIMOSA