Uncategorized

HATMA YA KICHUYA,NDEMLA, AJIBU NDANI YA SIMBA IPO HIVI

admin April 9, 2020 5:35 am


UONGOZI wa Simba umesema kuwa hatma ya wachezaji wote ndani ya kikosi hicho ni pale ambapo Ligi Kuu Bara itakamilika ndipo watataja wale watakaochwa na watakaoongezewa mikataba.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara ikiwa imesimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona kuna wachezaji ambao maisha yao kikosi cha kwanza yalikuwa magumu.

Nyota hao ni pamoja na Shiza Kichuya, Said Ndemla, Ibrahim Ajibu, Yusuph Mlipili.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingiza amesema kuwa kwa sasa itakuwa ngumu kuwataja wachezaji watakaochwa na watakaobaki ndani ya Simba.

“Bado ligi haijaisha licha ya kwamba kwa sasa imesimama, haitapendeza iwapo watatajwa wale watakaoachwa kwa muda huu itawaumiza hivyo acha maisha yaendelee,” amesema.

WACHEZAJI WA LIGI KUU ENGLAND WAUNDA UMOJA WAO KUPAMBANA NA CORONA MCHONGO WA NDINGA MPYA UMEFIKIA PATAMU, NI RAHISI SANA NUNUA CHAMPIONI AMA SPOTIXTRA GAZETI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply