Uncategorized

WACHEZAJI WA LIGI KUU ENGLAND WAUNDA UMOJA WAO KUPAMBANA NA CORONA

admin April 9, 2020 5:35 am


WACHEZAJI wa timu zinazoshiriki Ligi Kuu England wameunda umoja wao ambao una malengo ya kukusanya fedha kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kupambana na Virusi vya Corona.
Muasisi wa umoja huo ni nahodha wa Klabu ya Liverpool Jordan Henderson ambaye ameungwa mkono na mmakapteni wenzake ikiwa ni pamoja na Harry Maguire wa Manchester United.
Kwa sasa Ligi Kuu England imesimamishwa na inatarajiwa kurejea pale hali itakapokuwa shwari kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona ambao ni janga la dunia kwa sasa.
Mfuko huo ambao unawajumuisha wachezaji wote wanaoshiriki Ligi Kuu England umepewa jina la Players Together ambapo watashirikiana na Shirika la NHS kwa upande wa misaada pamoja na NHSCT.
Taarifa juu ya uwepo wa kundi hilo ilitolewa jana Jumatano ambapo wachezaji wamewapa majukumu manahodha wa timu zote kusimamia masuala ya makusanyo ya fedha ili kuongeza nguvu kwenye sapoti ya kupambana dhidi ya Corona.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTIXTRA ALHAMISI, NAFASI YA KUSHINDA NDINGA NI YAKO HATMA YA KICHUYA,NDEMLA, AJIBU NDANI YA SIMBA IPO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply