Home Uncategorized SERIKALI YAIPA BARAKA STARS, WAZIRI AIKABIDHI BENDERA

SERIKALI YAIPA BARAKA STARS, WAZIRI AIKABIDHI BENDERA


Serikali kupitia Naibu Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza imekabidhi rasmi  Bendera ya Taifa kwa Nahodha wa kikosi cha timu ya Tanzania ‘Taifa Stras, Mbwana Samatta, ambao wanaondokamapema kesho kwenda Misri kwa ajili ya michuano ya Afcon.


Stars imeagwa na waziri huyo ikiwa inaenda Misri kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) ambayo inatarajiwa kuanaanza Juni 21 mwaka huu nchini humo.


Stars itaondoka inatarajiwa kuondoka kesho  Ijumaa kuelekea Misri kwa ajili ya kambi ya wiki mbili kabla ya kuanza michuano hiyo rasmi ambapo kabla ya kuondoka kocha atataja kikosi chake ambacho kitaenda kupambana  kwenye michuano hiyo kabla ya safari kuanza hapo kesho.



Waziri Shonza alisema wanaimani kubwa na kikosi hicho  na kwamba  wanaamini kuwa Stars itaenda kufanya vyema na kama serikali wataendelea kuisapoti kwa nguvu zote hadi mwisho wa mashindano hayo.


“Tunaamini  kubwa na timu yetu itakayokwenda kupambana na kufanya vizuri  huko Misri, hivyo  tunamshukuru sana  rais wetu Dkt. John Magufuli kwa kuendelea kutupa sapoti kwa kila jambo na  ndiyo maana  utaona leo tunawaaga kwa niaba ya nchi hivyo hili la kuja  kuwaaga rasmi lilikuwa halikwepeki hasa ukilinganisha uwezo na sapoti  kubwa ya wananchi.



“Mbali na hili tungependa kuwaomba sana mkazingatie Suala la nidhamu na mshikamano kati yenu kwa sababu tunaamini mnaenda kuandika historian mpya kwa nchi hivyo niwaombe tu  mkapambane kufa na kupona alau muweze kumaliza hiyo michuano katika nafasi bora na sisi tutaendelea kuwasapoti kwa maombi na kila kitu,” alisema Shonza.

SOMA NA HII  BIASHARA UNITED YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA AZAM FC KARUME, MARA