Home Uncategorized VIDEO: MRITHI WA MAKAMBO KUTUA YANGA – VIDEO

VIDEO: MRITHI WA MAKAMBO KUTUA YANGA – VIDEO


Mshambuliaji nyota wa timu ya Taifa ya Namibia, Sadney Urikhob yuko katika hatua za mwisho kujiunga na Klabu ya Yanga.

Wakati Urikhob akijiandaa kutia saini mkataba na klabu hiyo, beki Gadiel Michael ametia saini mkataba wa miaka mitatu kuendelea kuitumikia Yanga.

Urikhob alitarajiwa kuwasili nchini Juni 4, 2019 usiku na kutia saini mkataba wa miaka miwili kabla ya kurejea katika kambi ya timu yake ya Taifa inayojiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) zinazotarajiwa kuanza Juni 21 hadi Julai 19.

Chanzo hicho cha habari kilisema Urikhob alishamalizana na mmoja wa viongozi wa Yanga akiwa nchini Namibia.
Rekodi za mshambuliaji huyo zinaonyesha aliwahi kucheza timu ya Amazulu ya Afrika Kusini, Saraburi,  Super Power Samut Prakan, BEC Tero Sasana (zote za nchini Thailand) na PSMS Medan ya Indonesia.

SOMA NA HII  DAVID MOLINGA HAKUPENDA KUSEPA NDANI YA YANGA